Msanii na muigizaji kutokea Tanzania, Lulu Diva amweka wazi kwamba yule mpenzi wake ambaye anaishi Uingereza na ambaye ndiye alivujisha video za utupu wake mitandaoni wiki jana si kijana wa rika lake bali ni mtu mzima mzee wa miaka 55.
Katika mahojiano ya simu aliyofanya na mtangazaji Soud Brown, Diva alisema kwamba alikuwa anajiachia wakiwa katika maongezi na huyo mpenzi wake kwani alikuwa anajua kutokana na umri wake uliokwenda, huenda ni mtu amekomaa kiakili na hangedhania kama angemfanyia kitu kama hicho.
Kibao kiligeuka na akalazimika kumeza ukweli kwamba si kila mzee unayemuona ana busara kwani wajinga nao huzeeka na kamwe hawabaki kuwa watoto, pale alipoamka na kupata taarifa za video zake za ponografia ndilo gumzo la mitandaoni na vijiweni.
Diva alisikika kwenye huo mkanda wa sauti akisema kwamba alikuwa tayari kutulia na mwanaume huyo kutokana na kwamba alikuwa anamuona jamaa katulia katika maisha hana papara za ujanani, na ndio maana alikuwa anajiachia huru raha mstarehe wakiwa wanafanya mambo yao.
Kingine alichokisema ni kwamba wakati wa kujiachia kote kule hakuwa na ufahamu kabisa kama mzee yule alikuwa anamrekodi na kisha kuja kutumia video zile dhidi yake kama mkuki, kwa sababu anasikika akisema baadaye alipouliza kwa nini anapakia, jibu la mwanaume yule lilikuwa ‘mimi nataka Lulu afe kabisa apotee katika uso wa dunia’ ebo!
Diva ameongeza kuwa ni muda kidogo tangu walipokuwa wapenzi na kuachana na alikuwa anajiachia mara kadhaa hivyo bado anafikiri ex wake huyo atakuwa na videos zake nyingine za faragha na hajui ataziachia lini
Lulu Diva amesema hakuna chochote kikubwa kuwa labda alifanyiwa na mwanaume huyo kimaisha ndio maana akamdhalilisha kusambaza videos zake za faragha. Awali, Lulu alisema aliachana nae baada ya kuona mwanaume amejaa sana wivu na muda mwingi anataka wazungumze kwa video call.
Kina dada mnaopendelea kuchumbiana na wqazee rika la baba zenu haya ndio yatawapata, sisi tupo hapa kuwapa pole tu!