Je wejua kwamba asilimia sitini ya mwili wa binadamu ni maji? Naam, mwili wa binadamu huhitaji takribani vikombe 6 vya maji kila siku ambazo ni lita mbili.
Unywaji wa maji una faida nyingi na husaidia mwili katika kupambana na maradhi, Maji hutengenezaji wa mate, usafirishaji wa virutubisho, na udumishaji wa joto mwilini.
Hizi hapa ni faida 8 za kiafya zinazotokana na kunywa maji.
1. Matatizo ya choo. Maji ni dawa ya kutibu ugumu wa kwenda haja kubwa, kunywa maji ya kutosha kila siku na utajiepusha na tatizo la ukosefu wa choo mara kwa mara.
2. Usafishaji wa mwili. Maji husaidia katika kuondoa sumu mwilini kwa kutoa uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa.
3. Kupunguza uzani. Ukiwa wataka kupunguza uzani basi kunywa maji kwa wingi kwani maji hayana mafuta wala sukari.
4.Pia maji husaidia katika usafishaji wa mwili. Maji huondoa sumu na uchafu mwilini kwa kutoa uchafu wote kwa njia ya mkojo na haja kubwa.
5. Maji ni tiba ya kichwa kuuma. Dalili ya kupungukiwa maji mwilini ni kuumwa na kichwa.Wataalamu wa afya wanashauri watu kunywa maji ya kutosha na hautasumbuliwa sana na kmaimuvu ya kichwa mara kwa mara.
6. Maji Nishati ya mwili kwani Mwili unapopungukiwa na maji, hukufanya ujihisi mchovu, hivyo kwa kunywa maji ya kutosha kila siku utakuwa mwenye nguvu. Binadamu anahimizwa kunywa maji badala ya vinywaji baridi kama vile soda, juisi au bia.
7. Unywaji wa maji utakufanya ngozi yako kuwa nyororo na ya kupendeza.Maji husafisha ngozi yako na kutoa uchafu kama jasho.
8. Afya ya moyo. Unywaji wa maji ya kutosha unaweza kupunguza hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo. Utafiti unaonyesha kuwa watu wanaokunywa glasi ya maji zisizopungua 5 kila siku hujiepusha na uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo kwa asilimia 41 zaidi ya wale wanaokunywa glasi 2.
Hivyo kila mtu analojukumu la kulinda mwili kuhakikisha hamenyani na magonjwa hayana dawa au asili.