logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kijana wa miaka 20 afariki wakati wa ubatizo baada ya kutumbukizwa majini mara 14

Polisi wanamshikilia mchungaji wa kanisa hilo la New FoundationChurch of Jerusalem.

image
na Radio Jambo

Football26 July 2023 - 11:47

Muhtasari


• Babake marehemu alisema kuwa anashangaa ni kwa nini walimpeleka mwanawe saa kumi na moja jioni kwenye mto kumbatiza peke yake.

Rip

Maafisa wa polisi wamelazimika kuaznisha uchunguzi baada ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 20 kuripotiwa kuaga dunia akiwa mikononi mwa mchungaji wakati wa ubatizo wake.

Kwa mujibu wa blogu ya Zambian Observer kama ilivyoripotiwa na kituo kimoja cha redio nchini himo, kijana huyo alifariki wakati wa kubatizwa kwake baada ya kutumbukizwa majini mara 14 kwa mfululizo.

Polisi wanamshikilia mchungaji wa kanisa hilo la New FoundationChurch of Jerusalem.

Baba wa marehemu Robson Mooya alithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa Wave FM na kumtaja mtoto wake aliyefariki kuwa ni Oneell Mooya, blogu hiyo iliripoti.

Bw Mooya anaeleza kwamba alimpeleka mwanawe ambaye alikuwa akilalamika kuumwa kichwa kwa waumini wa kanisa hilohilo kwa ajili ya maombi kisha baadaye akarudi nyumbani kwenda kuleta chakula.

Anadai kwamba nyuma na bila wasiwasi wake washiriki hao 3 wa kanisa lililotajwa walimpeleka mtoto wake kwenye bwawa la Filiot karibu 17:20 kwa ubatizo ikiwa alikufa baada ya kuzamishwa mara 14 kwenye maji – taarifa Zaidi ilieleza.

Bw Mooya ameshangaa ni kwa nini washiriki hao walimchukua mwanawe kwa ubatizo hadi saa kumi na moja bila washiriki wengine wa kanisa waliokuwepo wakati wa ubatizo huku wakishangaa zaidi kwa nini mwanawe alibatizwa peke yake.

Anaongeza kuwa watu hao walipofikishwa polisi walidai walimkuta marehemu akiwa amekufa kwenye Bwawa hilo ambalo baadaye lilithibitishwa na polisi kuwa si kweli.

Mwili wa marehemu ulizikwa Julai 25 baada ya uchunguzi wa maiti.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved