Seneta wa Kaunti ya Vihiga Godfrey Osotsi amesema kuwa uchaguzi wa FKF unaotarajiwa kufanyika tarehe 7 Desemba tayari umeibwa.
Seneta Osotsi amesema hayo katika bunge la seneti mnamo
Jumatano tarehe 30, akitoa maoni kuhusu kauli ya Seneta mteule Catherine Mumma
kuhusiana na soka la nchini.
Kwa mujibu wa seneta Osotsi, kauli ya seneta Mumma
imejitokeza kwa wakati unaostahili kwani sekta ya soka nchini itakuwa inafanya
uchaguzi wake hivi Karibuni.
Osotsi amesema kuwa bodi ya kusimamia uchaguzi huo
iliteuliwa na viongozi walioko mamlakani kwa sasa hivyo basi matokeo ya
uchaguzi huo huenda yakawa kinyume na matokeo halisi.
“Uchaguzi huu tayari umeibwa kwa sababu ofisi ya sasa ndio iliteua watu
watakaoendesha uchaguzi huo na kama hivyo ndivyo kulivyo basi matokeo yatakuwa
kwa upendeleo wao.” Alisema
seneta Godfrey Osotsi.
Seneta huyo alisema kuwa uongozi wa sasa umewaangusha
Wakenya katika kukuza soka la Kenya.
Seneta Osotsi pamoja na baadhi ya maseneta wengine
wamesisitiza haja ya kuwepo kwa uongozi wa watu walio na tajriba kuendesha soka
la humu nchini akisema kuwa tatizo linaloikumba sekta ya michezo nchini
makampuni ambayo yamejiingiza katika soka, raga, riadha na michezo mingine.
“Hii nchi ina uwezo wa kufanya vyema katika michezo haswa kabumbu
lakini kwa sababu tumeruhusu watu wasio na uelewa wa soka kuendesha sekta hiyo
ndio wanasimamia soka.” Aisema Osotsi.
Awali, seneta Mumma alitaka kamati ya leba na ustawi wa jamii
ya bunge la seneti kutoa ripoti kuhusu utiifu wa kananu zinazosimamia shirikisho
la soka nchini FKF na katiba ya Kenya.