logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mathare United yawaadhibu wachezaji wake 4 kwa utovu wa nidhamu

Wachezaji hao walikiuka vipengee kadhaa vya mkataba baina yao na klabu hiyo

image
na Brandon Asiema

Football30 October 2024 - 17:04

Muhtasari


  • Mathare United imewapa adhabu ya kukosa mshahara wa wiki mbili kutoka Jumatano Oktoba 30.

caption

Mathare United imewaadhibu wake wanne kwa utovu wa nidhamu baada ya kukiuka sheria ya mkataba baina yao na klabu hiyo.


Klabu hiyo imeafikia kuwachukulia hatua ya nidhamu wachezaji Kevin Kimani, Elli Asieche, Brian Ouru na Eric Mulu  baada ya kushiriki katika mashindano mengine wakichezea timu nyingine bilaya rukhusa ya klabu walioweka mkataba nao.


Taarifa ya usimamizi wa Mathare United imesema kwamba wane hao walichezea timu nyingine ambayo haijatajwa kabla ya Mathare kucheza mchuano wao wa sita wa ligi dhidi ya Police FC.


Wachezaji waliopatikana na utovu wa nidhamu wameadhibiwa kukosa mshahara wa wiki mbili kuanzia Jumatano ya tarehe 30, Oktoba.


Uamuzi wa mwisho wa Mathare United kuhusu swala hiyo umetolewa timu hiyo ikisema kuwa wachezaji hao walivunja vipengee kadhaa katika mkataba ikiwemo kukosa  kuweka viwango vya juu vya ubora wa mwili wakati wote.

Vile vile usimamizi wa Mathare United umesema kuwa wachezaji hao walikiuka mkataba kwa kushiriki katika michezo mingine inayoweza hatarisha ubora wa mili yao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved