Manchester United yapata ushindi wake wa kwanza chini ya kaimu kocha Ruud van Nistelrooy katika taji la Carabao dhidi ya timu ya Leicester City katika raundi ya 16 katika uga wao wa nyumbani wa Old Trafford mechi iliyochezwa tarehe 30 Oktoba.
Ruud van Nistelrooy alijivunia ushindi huo mnono wa mabao 5-2 huku wakitinga katika hatua ya robo fainali.Mancher United sasa watamenyana na timu ya Tottenham Hotpur.
Kwingineko ni kuwa klabu ya Tottenham Hotpur waliweza kuwaduwaza vijana wa Pep Guardiola Manchester City mabao 2-1 katika uga wao wa nyumbani na kukata tiketi ya kucheza katika hatua ya robo fainali.
Arsenali vile vile waliweza kufika hatua ya robo fainali baada ya kuwapiga Preston North-End wanaoshiriki daraja la pili Uingereza.Mabingwa watetezi Liverpool, wako mbioni kutetea taji hilo mara nyingi baada ya kupata ushindi na kufika hatua ya raundi ya 8.
Kwenye taarifa zinazofungamana na uhamisho wa kocha Ruben Amorimi ni kuwa ripoti zinaashiria kuwa bado atasalia kwa mechi tatu zijazo za timu hiyo ya Sporting kabla ya kukamilisha usajili rasmi kuingia United.Aidha, Amorimi atajiunga na United katika mapumziko ya mwezi Novemba.
Vijana wa Enzo Maresca walionyeshwa kivumbi wakiwa ugenini huku Newcastle wakilipiza kisasi. Chelsea walionekana kutokuwa na utulivu katika mechi hiyo na vijana hawa wa Eddie Howe kuonyesha mchezo wa haiba na kutia shinikizo kwa chelsea.Newcastle walipata mabao kupitia Alexander Isak na bao la kujifunga la Axel Disasi.