logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Song ateuliwa kuwa kocha wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Song mwenye umri wa miaka 48 anachukua nafasi ya Mswizi Raoul Savoy.

image
na BBC NEWS

Football15 January 2025 - 07:13

Muhtasari


  • Song aliiongoza Indomitable Lions kwenye michuano ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar na Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka jana.


Beki wa zamani wa Liverpool na West Ham Rigobert Song ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).

Song mwenye umri wa miaka 48 anachukua nafasi ya Mswizi Raoul Savoy, ambaye alitimuliwa Oktoba kuelekea mwisho wa kampeni ya CAR ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 (Afcon) 2025.

Song, ambaye aliichezea Cameroon mara 137 katika kipindi cha miaka 17 ya soka lake la kimataifa aliwahi kuongoza timu ya soka ya nchi yake kwa miaka miwili.

Nyota huyo wa soka wa zamani aliiongoza Indomitable Lions kwenye michuano ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar na Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka jana, ambapo timu hiyo ilitolewa katika hatua ya 16 bora.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved