Kesi iliyosubiriwa kwa muda mrefu ya wahudumu wa matibabu waliomtibu gwiji wa soka wa Argentina marehemu Diego Maradona imeanza katika mji mkuu, Buenos Aires.
Maradona alikuwa akiendelea kupata nafuu alipofariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa nyumbani kwake mwaka wa 2020, akiwa na umri wa miaka 60. Alikuwa akipata nafuu nyumbani baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuganda kwa damu kwenye ubongo mapema mwezi huo.
Waendesha mashtaka wanadai kuwa kifo cha Maradona kingeweza kuepukwa na kuwashutumu wafanyakazi wa hospitali hiyo kwa uzembe wa kiafya.
Washtakiwa wanasema Maradona alikataa matibabu zaidi na alipaswa kukaa hospitalini kwa muda mrefu baada ya upasuaji wake.
Wanakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka minane na 25 ikiwa watapatikana na hatia kwa shtaka la "mauaji ya kukusudia".