logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mmiliki wa Manchester ataja wachezaji wasioleta manufaa kwa timu licha ya mshahara mkubwa

Cha kushangaza ni kwamba, alifikia hatua ya kuwataja wachezaji watano wa United wakati wa kujadili uhamisho wa wachezaji.

image
na Japheth Nyongesa

Football12 March 2025 - 10:21

Muhtasari


  • Maamuzi kadhaa yaliyofanywa na Ratcliffe na washirika wake yamethibitisha kuwa hayapendezi kwa kila mtu.
  • wakati wa mazungumzo haya ndipo alipoelezea makosa kadhaa ambayo yamefanyika katika soko la uhamisho.

Mmiliki mwenza wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe amehoji waziwazi usajili wa wachezaji kadhaa wa sasa kaika timu ya Manchester United, akisema wamenunuliwa wakati wengine wamerithiwa na wanahitaji hali zao kushughulikiwa.

Bilionea huyo mkuu wa INEOS ametekeleza mabadiliko makubwa Old Trafford, na kumfukuza Erik ten Hag kama meneja baada ya awali kumpa mkataba wa kuongeza mkataba kabla ya kukatiza mamia ya ajira katika klabu hiyo kwa lengo la kupunguza gharama.

Ratcliffe, ambaye ni shabiki wa Manchester United, alishiriki katika mahojiano mengi siku ya Jumatatu na wanahabari. Na wakati wa mazungumzo haya ndipo alipoelezea makosa kadhaa ambayo yamefanyika katika soko la uhamisho, akidai sasa ni jukumu lake kusaidia kuondoa makosa ya wale waliotangulia mbele yake.

Cha kushangaza ni kwamba, alifikia hatua ya kuwataja wachezaji watano wa United wakati wa kujadili uhamisho wa wachezaji, watatu kati yao bado wanachezea klabu hiyo kwa sasa.

"Ukiangalia wachezaji tunaowanunua msimu huu, ambao hatungepaswa, tunanunua Antony, tunanunua Casemiro, tunanunua Onana, tunanunua Hojlund, tunanunua Sancho. Haya yote ni mambo yaliyopitwa na wakati zamani, iwe tunaipenda au la, tumerithi vitu hivyo na tunapaswa kutatua hilo.

"Kwa Sancho, ambaye kwa sasa anaichezea Chelsea na tunalipa nusu ya mshahara wake, tunalipa pauni milioni 17 kumnunua msimu wa joto.

"Baadhi ya wachezaji  sio wazuri na wengine huenda wanalipwa mishahara ya ziada, lakini kwa sisi kuunda kikosi ambacho tunawajibika kikamilifu na kuwajibika, itachukua muda," Ratcliffe aliendelea.


"Tuna kipindi hiki cha mabadiliko ambapo tunafahama kutoka zamani hadi siku zijazo. Kuna baadhi ya wachezaji wazuri katika kikosi kama tunavyojua, nahodha ni mchezaji mzuri. Kwa kweli tunahitaji Bruno, ni mchezaji mzuri."Alisema:

Maamuzi kadhaa yaliyofanywa na Ratcliffe na washirika wake yamethibitisha kuwa hayapendezi kwa kila mtu, lakini amekuwa akisisitiza kwamba ili kuimarisha heshima tena, United lazima ibadilishe kabisa jinsi wanavyofanya kazi na kufanya biashara.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved