logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wachezaji muhimu wa Man United watakaokosekana dhidi ya Real Sociedad usiku wa leo kwenye Europa

Ruben Amorim ametoa taarifa za hivi punde katika kikosi chake kabla ya mechi ya raundi ya pili ya ligii ya Europa raundi 16.

image
na Japheth Nyongesa

Football13 March 2025 - 11:23

Muhtasari


  • Orodha iliyopo ya wachezaji ambao hawatakuwepo kutokana na majeraha ni pamoja na Altay Bayindir, Tom Heaton, Jonny Evans, Lisandro Martinez, Luke Shaw, Kobbie Mainoo na Amad Dialo.
  • Mshambuliaji chipukizi Chido Obi hastahili kushiriki mashindano haya.

caption

Mkufunzi wa Manchester United Ruben Amorim ametoa taarifa za hivi punde katika kikosi chake kabla ya mechi ya raundi ya pili ya  ligii ya Europa raundi 16 dhidi ya Real Sociedad usiku wa leo 13 Machi.

Wekundu hao  wanaingia uwanjani Old Trafford wakiangalia uwezekano wa kufanya kazi hiyo kwa umakini ili kuvuna ushindi utakaowaelekeza kwenye robo fainali, kufuatia sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Reale Arena wiki iliyopita.

Kulikuwa na habari za kupeana morali kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya viungo Mason Mount na Manuel Ugarte kushiriki katika mazoezi wiki hii.

Lakini Leny Yoro amekosekana mazoezini, baada ya kushindwa kuonekana tena kwa kipindi cha pili cha sare ya 1-1 dhidi ya Arsenal wikendi iliyopita huku Amorim akiwa ametilia wasiwasi juu ya jeraha la mguu katika mkutano wa waandishi wa habari baada ya mechi hiyo ya Jumapili.

" Mason Mount ni wa haraka sana," alithibitisha Ruben katika Carrington. "Leny [Yoro] alikuwa nje. Harry Maguire hawezi kucheza mchezo huu. Nina matumaini ya kuwa naye Jumapili (dhidi ya klabu yake ya zamani Leicester City katika Ligi Kuu ya England).

"Manu [Ugarte] yuko kwenye kikosi na nadhani hakuna mtu anayerejea kwenye majeraha.

"Hapana, hakuna [kutokuwepo kwa Yoro] sio muda mrefu. Leny hawezi kucheza mchezo huu na mchezo mwingine [Leicester]."

Orodha iliyopo ya wachezaji ambao hawatakuwepo kutokana na majeraha ni pamoja na Altay Bayindir, Tom Heaton, Jonny Evans, Lisandro Martinez, Luke Shaw, Kobbie Mainoo na Amad Dialo

Mshambuliaji chipukizi Chido Obi hastahili kushiriki mashindano haya, lakini Harry Amass na Jack Fletcher ambao walifanya mazoezi na kundi hilo la timu kubwa siku ya Jumatano, wamesajiliwa na huenda wakajumuishwa kwenye kikosi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved