Chelsea inayaoshiriki katika ligi kuu ya Uingereza walipayta ushindi wa kuridhisha katika pambano la UEFA conference league dhidi ya timu ya Ugiriki Panathinaikos.
Chelsea walishinda ushindi wa mabao 4-1 wakiwa ugenini siku ya Alhamisi 24 Mwezi wa Kumi.The Blues walipata mabao yao kupitia wachezaji ,Jaoa Felix aliyepachika mabao mawili,Mykhailo Mudryk ambaye alifunga na kutoa pasi mbili zilizozalisha mabao na hatimaye Christopher Nkunku kufunga bao la nne kupitia mkwaju wa penati.
Kwingineko ni kuwa klabu ya Manchester united ilitoka sare ya bao 1-1 wakicheza na timu ya Fenarbahce katika pambano la Ueropa league.Aidha, katika pambano kocha wa zamani wa timu hiyo ya Man United, Jose Mourinho,alionyeshwa kadi nyekundu katika mechi hiyo.
Manchester United walipata bao la kuongoza kupitia mchezaji Christian Ericksen kabla ya mchezaji kutoka taifa la Morocco Youssef En-Nesyri kusawazisha kunako dakika ya 49 na kupelekea mechi hiyo kumalizika sare.
