logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Real Madrid, Man City na Bayern Munich njia panda kufuzu moja kwa moja raundi ya 16 bora klabu bingwa Ulaya

Miamba hao wapo katika mabano ya kucheza mechi za maondoano ya nyumbani na ugenini ili kufuzu hatua ya 16 bora

image
na Brandon Asiema

Kandanda13 December 2024 - 08:38

Muhtasari


  • Aston Villa, Arsenal na Liverpool wapo ndani ya mabano ya kufuzu moja kwa moja katika hatua ya 16 bora zikiwa timu za ligikuu ya Uingereza zinazofanya vyema kwenye klabu bingwa barani Ulaya.
  • Kufikia Ijumaa Disemba 13, timu zote 36 zimebakisha mechi mbili kwenye hatua ya makundi za kuzisaidia kutinga hatua ya kumi na sita bora.


Vilabu vikubwa barani Ulaya vyenye ueledi katika kipute cha klabu bingwa barani Ulaya huenda zitakosa fursa ya kufuzu moja kwa moja katika hatua ya kumi na sita bora kwenye kipute cha klabu bingwa barani Ulaya msimu 2024/2025.

Katika mfumo mpya wa kipute hicho unaochukua mkondo wa ligi licha ya timu kuwa kwenye makundi mbali mbali, jumla ya timu 36 zinashiriki makala ya msimu huu ambapo vilabu vitakavyomaliza ligi hiyo katika nafasi za kwanza 8, zitafuzu moja kwa moja kwa hatua ya 16 bora.

Timu ambazo zitamaliza katika nafasi ya kati ya 9 na 24, zitafanyiwa droo ambapo timu mbili mbili zitakutana katika mechi ya nyumbani na ugenini ambako mshindi atajiunga na timu za nane kwanza katika hatua ya 16 bora. Timu ambazo zitakosa katika nafasi za kwanza 24, zitabanduliwa rasmi kutoka kwenye mashindano hayo.

Kufikia Ijumaa Disemba 13, timu zote 36 zimebakisha mechi mbili kwenye hatua ya makundi za kuzisaidia kutinga hatua ya kumi na sita bora.

Hata hivyo baadhi ya timu tayari zimkosa kufuzu hatua ya kumi na sita bora kutoka na matokeo duni walioweka. RB Leipzig, Bologna, Young Boys na  SK Slovan Bratislava tayari zimekosa kufuzu kwa hatua ya 16 bora ikiwa zinasalia mechi mbili kwenye hatua ya makundi.

Aidha timu nyingine kubwa katika ligi za Ulaya pia, zinakabiliwa na tishio la kukosa kufuzu hatua ya 16 bora. Baadhi ya timu hizi ni mabingwa mara nne mfululizo wa ligi ya Uingereza Man City, mabingwa watetezi wa kombe hilo Real Madrid pamoja na miamba wa soka wa Bundesliga Bayern Munich.

Baada ya raundi ya sita ya mechi za makundi timu tajika barani Ulaya ikiwemo Bayern Munich, Borrussia Dortmund, AC Milan, Real Madrid, Man City, Juventus na Atletico Madrid zipo katika mabano ya kushiriki mechi za muondoano ili kutinga raundi ya kumi na sita bora.

Aston Villa, Arsenal na Liverpool wapo ndani ya mabano ya kufuzu moja kwa moja katika hatua ya 16 bora zikiwa timu za ligikuu ya Uingereza zinazofanya vyema kwenye klabu bingwa barani Ulaya.


Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved