
Mashindano hayo, ambayo hapo awali yalipangwa kuanza Aprili 26 hadi Mei 18, sasa yanakabiliwa na changamoto huku Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) likitarajiwa kutangaza ukumbi mbadala.
Uamuzi huo wa kushangaza ulioripotiwa na serikali ya Ivory Coast na kuthibitishwa na shirikisho la soka la nchi hiyo (FIF). Katika taarifa rasmi rais wa FIF Yacine Idriss Diallo alisema:
"Yacine Idriss Diallo, Rais wa Shirikisho la Soka la Ivory Coast na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya U20, tunakufahamisha kwamba serikali imearifu Shirikisho la Soka la Ivory Coast, kupitia barua rasmi, kuhusu kujiondoa kwa Ivory Coast kuwa nchi mwenyeji wa AFCON ya U20."
"Kwa mujibu wa maagizo ya Rais wa Shirikisho, mkurugenzi mtendaji aliwasilisha habari hii kwa Katibu Mkuu wa CAF Jumanne, Machi 25." Dialo alieeleza.
Rais wa michezo wa nchi hiyo aliwashukuru wale ambao walikuwa wamehusika na kuendelea kujipanga kwenye maandalizi hayo.
"Rais angependa kutoa shukrani zake za dhati kwa kila mtu kwa kujitolea kwake na juhudi zilizofanywa katika kuandaa mashindano haya. Pia anawahakikishia wadau wote kwamba CAF itatoa sasisho zaidi juu ya jinsi hali hii itakavyoshughulikiwa.
Timu ya taifa la Kenya ni miongoni mwa timu za Afrika ambazo zinatarajiwa kushirika kwenye mapambano hayo. Kenya ilipangwa katika Kundi C, na itaanza kutetea taji hilo dhidi ya Zambia, senegal, na Sierra Leone. Kunndi ambalo ni lenye ushindani mkali.
