logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Pumzika vyema mpenzi!" Wema Sepetu amkumbuka aliyekuwa mpenziwe Steven Kanumba

Katika kipindi cha mahusiano yao, Wema alipata ujauzito mara mbili na kuutoa kila mar

image
na Radio Jambo

Michezo07 April 2022 - 11:00

Muhtasari


•Wema ambaye pia amewahi kuwa kwenye mahusiano na Diamond Platnumz alimtakia marehemu Kanumba mapumziko mema peponi.

•Katika kipindi cha mahusiano yao, Wema alipata ujauzito mara mbili na kuutoa kila mara, jambo ambalo anaamini linamwathiri hadi wa leo.

Mwigizaji mashuhuri wa Bongo Wema Sepetu ameadhimisha miaka kumi tangu kifo cha aliyekuwa mpenzi  wake Steven Kanumba.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema alifufua kumbukumbu zake na mwigizaji huyo kwa msururu wa picha.

Wema ambaye pia amewahi kuwa kwenye mahusiano na Diamond Platnumz alimtakia marehemu Kanumba mapumziko mema peponi.

"Siwezi kuamini mwongo umepita.. Mwongo hivo tu.. Rest Easy Booboo," Wema aliandika chini ya picha zake na Kanumba.

Wema na Kanumba walichumbiana kwa kipindi kisichothibitishwa kabla yao kutengana katika hali tatanishi.

Katika kipindi cha mahusiano yao, Wema alipata ujauzito mara mbili na  kila mara kuutoa, jambo ambalo anaamini limemwathiri hadi wa leo.

Takriban miaka miwili iliyopita, Wema alikiri kuwa kuavya mimba ya kwanza ilikuwa ni makubaliano kati yao wawili ila ya pili ilifanywa kwa siri bila Kanumba kujua.

Kanumba alifariki mnamo Aprili 12, 2012. Kwa wakati huo alikuwa anachumbiana na mwigizaji Elizabeth Michael ambaye alishtumiwa kuhusika na kifo chake na kushtakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved