William Makali alikuwa mwanawe makamu wa Rais marehemu Kijana Wamalwa.
Waziri huyo alisema kuwa William aliaga dunia jumapili jioni baada ya kukimbizwa hospitalini kupata matibabu.
Eugene aliongeza kuwa William alikuwa buheri wa afya siku ya jumamosi na hata alishinda na marafiki wake, lakini siku ya jumapili alipatikana nyumbani kwake kama amepoteza fahamu.
Vile vile alisema famila itatoa ripoti ya sababu cha kifo chake baada ya kutolewa kwa postmoterm.
William alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Nairobi.
