"Nilikuwa najitayarisha kuzindua video mpya, nilipoteza kazi zangu zote mwaka wa 2015, nilikuwa nafanya kazi katika vituo viwili vya radio na kufanya kipindi kimoja katika runinga.Nilikosa kipindi kimoja cha runinga kwa sababu ya maumivu ya hedhi, nilihakikisha waajiri wangu walijua maumivu yangu kwa hivyo nilikuwa napewa ruhusa ya siku saba kila mwezi.
Kuna wakati nilikosa kipindi kimoja lakini mtayarishi hakutaka kujua hali yangu, kwa hivyo nilifutwa kazi kwa ajili ya kukosa kipindi kimoja, muda huo wote sikufahamu nilikuwa na maradhi ya Endometriosis
Nilijaribu kutilia maanani kazi yangu ya redio lakini singeweza kwa maana afya yangu ilikuwa inazidi kudorora na kunifanya nyonge kutoweza kupanza ngazi.Mazoea ya kampuni za habari kufuta watu kazi yalijiri na nikawa miongoni mwa watu 200 waliofutwa kazi, nilichukuwa barua yangu na kuelekea nyumbani." Alieleza Koikai.
Alizidi kunakili ujumbe wake na kusema,
"Huu ni msimu wa ajabu na mwema kuweni na imani, na muwe na matumaini mna talanta nyingi ambazo hazijulikani,shukuruni Mungu kwa ajili ya mitandao ya kijamiiMnaweza kufanya kazi kupitia mitandao Mungu yupo katika kiti chake cha enzi na ana shughulikia hali yenu."
Chamno Koikai baada ya kufutwa kazi alikumbana na haya;
"Kama vile nyinyi nyote mwafahamu nililelewa na nyanya yangu na mama yangu wakati huo nilifutwa kazi nilienda nyumbani na kumpata nyanya yangu akiwa na maumivu ya tumbo.Baada ya wiki mbili alipatikana na saratani ya kongosho, pia hali yangu ilikuwa inazidi kudhoofika nilipofanyiwa vipimo nilipatikana na Endometriosis.
Pia sauti yangu ilikuwa inazidi kupotea namshukuru @SELECTORTECHNIX ambaye alisimama na mimi hadi sasa.
Kwa miaka mitano sijakuwa katika kazi nzuri, nimepigana na hali ya afya yangu kwa muda hospitalini, nilirejea nyumbani mwaka jana ili kujiendeleza kimaisha lakini virusi vya covid-19 nikavuruga mipngo yangu lakini bado nina matumaini
MHARIRI: DAVIS OJIAMBO
