Kuna wakati wanawake wa Kenya walipokuwa wanaona ngozi nyeupe yaa ni mzungu wanamwaga mate kwa ajili walijua kwamba ni pesa ambazo atakuwa akiongea nazo.
Licha ya wazungu kuchanuka na kufahamu kuwa kuna baadhi ya wanawake ambao wanataka tu pesa bali si mapenzi wamezidi na kutapeliwa na wanawake hawa kila kuchao.
Kuna baadhi ya hila ambazo wanawake hutumia kuwanasa wazungu, na hila hizo nikama vile zifuatavyo;
1.Mpenzi nina mimba yako
Kama mwanamke anahitaji pesa ili kufanikisha maisha yake atafanya chochote ili kunasa mzungu na kula pesa zake pole pole.
Kuna wale watadai wana ujauzito wao ili wapate pesa kutoka kwa mzungu huyo.
2.Mimba yangu ilitoka mapema
Baada ya kula pesa zake na kuacha akipepeta mikono na unataka kumuacha kuna wale watasimama kidete na kumwambia kwamba ujauzito wake ulitoka mapema.
3.Nataka unioe
Kuna wale wavuka mipaka na kutaka waolewe na mzungu kwa ajili ya pesa zake, kisha akitajirika au akiomoka haya basi mzungu utaahwa pekeyako na mapenzi yataisha.
4.kuwa mwenzangu wa kibiashara
PIa kuna wale watawasihi wafanye biashara pamoja na endapo amepata alichokuwa anataka anamtema mzungu huyo.
Tabia kama hizi zitaachwa lini na kisha kama wanawake tujipe heshima zetu.
Si wote ambao utawaona na wazungu watakuwa wakitaka pesa bali watakuwa wakitafuta mapenzi ya kweli, lakini kwa maana kuna wale waliaharibu jina kitambo weng watafikiria anatafuta tu pesa.
