logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ray C amjibu Lady Jaydee kwa kauli yake kuhusu matumizi ya dawa za kulevya

Ray C alimkumbusha Jaydee kuwa yeye ni mama licha ya kuwa mraibu.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri14 December 2023 - 08:25

Muhtasari


• Ray C ambaye miezi michache iliyopita aliweka wazi kupata mtoto wake wa kwanza, wengi wanajua historia yake ndefu jinsi uraibu wa dawa za kulevya.

Ray C na Lady Jaydee

Malkia mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amemjibu msanii mwenzake Lady Jaydee baada ya kutoa kauli kuhusu dawa za kulevya katika ukurasa wake wa X.

Lady Jaydee awali alikusudiwa kuwa kauli hiyo yake ilikuwa inamlenga msanii mwenzake mkongwe, Chid Benz ambaye Jumanne wiki hii alifanya mahojiano na kukiri kwamba anapitia maisha magumu sana licha ya ngoma zake kutamba katika miaka ya mapema ya 2000s.

Chid Benz katika mahojiano hayo na kituo kimoja cha redio nchini Tanzania, alimshauri Lady Jaydee kuanza kumtumikia Mungu kwa nyimbo za injili, baada ya kuburudisha mashabiki kwa nyimbo za sekula kwa Zaidi ya miono miwili sasa.

Jaydee kwa kile kilikisiwa kuwa ni jibu kwa kauli ya Benz, alikwenda kwenye X na kuandika kauli ya kumshukuru Mungu kwa kumuepusha kutokana na dawa za kulevya ambazo zimewazamisha wasanii wengi akiwemo Chid Benz na Ray C miongoni mwa wengine.

Nashukuru Mungu alinipa ujasiri wa kukabili mapito yangu bila kuingia kwenye biashara za kula Unga na kuanza kumlaumu kila mtu. Lord i thank you,” Jaydee aliandika na kumalizia kwa emoji ya shukrani.

Wakati wengi wanadhani kauli hii ilikuwa inamlenga moja kwa moja Chid Benz, Ray C alichomoka ghafla na kumjibu Jaydee akisema kwamba licha ya kudharauliwa kwa kuzama katika matumizi ya dawa za kulevya, leo hii yeye ni mama, na kusema kwamba Mungu habagui kwani waja wote ni wake – wanaotumia dawa za kulevya na wasio tumia.

Pamoja na yote niliyopitia Mungu wangu hakusita kuniinua tena na kunipa zawadi juu leo hii Naitwa MAMA😍.I thank you God..Funzo……Mungu ni wetu sote,” Ray C aliachia maoni yake kwenye ukurasa wa Instagram wa mtangazaji Millard Ayo ambaye alikuwa amechapisha kauli hiyo ya Jaydee.

Ray C ambaye miezi michache iliyopita aliweka wazi kupata mtoto wake wa kwanza, wengi wanajua historia yake ndefu jinsi uraibu wa dawa za kulevya uliizamisha taaluma yake ya muziki.

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved