Kulingana na Anthony, alikuwa na mpango wa kando jambo ambalo lilipelekea wawili hao kutengana na isitoshe, bwana huyu alipata mtoto na mwanamke huyo.
Kituko kilizuka wakti bwana huyu alifichua kuwa alikuwa na mipango ya kufanya harusi mwezi wa Disemba lakini mamake mzazi hampendi mwanadada huyo aliyewatenganisha Anthony na Lucy, kisa na maana ni mvivu na asiyeshughulikia mumewe.
"Mamangu aliniarifu kuwa hataki mwanadada huyo niliyekuwa na mpango wa kando naye, kwani ni mvivu na hamsaidii na kazi za nyumbani ikilinganishwa na Nancy ambaye ana bidii ya mchwa." Alijieleza Anthony.
Alipopigiwa simu, Nancy ambaye bado alikuwa usingizini alikataa katakata kurudiana na Anthony huku akiomba mda zaidi kufikiria.
Kulingana na Nancy, lazima wazazi wa Anthony wakazungumze na wazazi wake kabla yake kuamua, huku akifichua kuwa sio mpango wa kando tu uliowasambaratisha bali kuna mengi kama kutusiwa akiwa kwa ndoa.
Skiza kanda ifuatayo.
&feature=youtu.be