logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanaume mmoja wa miaka 30 ajitoa uhai baada ya mkewe kutoweka na pesa Sh38,000

Mwanaume mmoja wa miaka 30 ajitoa uhai baada ya mkewe kutoweka na pesa Sh38,000

image
na

Habari01 October 2020 - 16:11
Mwanaume mmoja kwa jina Livingstone Obudi mwenye umri wa miaka 30 katika kaunti ya Siaya amejitoa uhai baada ya mkewe kutoweka na pesa zake shilingi 38,000 kutokana na mzozo wa kifamilia.

Marehemu aliye chukulia ngovi baina yake na mkewe kama jambo la kawaida na kuenda matembezi baada ya ungovi, alipigwa na butwaa aliporejea jiono na kumkosa mkewe pamoja na pesa zake na kuamua kujitoa uhai kwa kunywa sumu.

Inadaiwa kuwa mkewe marehemu alifunganya virago baada ya ugomvi na mmewe kabla ya kutoweka na shilingi 38,000 ambazo marehemu alikuwa amehifadhi kwa mjibu wa ujenzi.

juhudi za kumkimbiza marehemu katika hospitali ya rufaa ya Kisumu hazikufua dafu baada ya kufariki pindi alipofika katika chumba cha wagonjwa mahututi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved