Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayotarajiwa kupokea chanjo ya Covid 19 kufikia mwisho wa mwezi huu kulingana na COVAX .
Katika ripoti iliyotolewa siku ya jumatano Kenya imeorodhesha kuwa miongoni mwa nchi ambazo zitapokea chanjo hioyo kulingana na utaratibu wa matumizi ya dharura wa WHO .
Kenya itapokea dozi 4,176,000 Uganda itapokea 3,552,000 ilhali Rwanda itapokea dozi 996,000 .
Somalia itapokea dozi 1,224,000 ilhali sudan itapokea dozi 3,396,000 nayo sudan kusini itapewa dozi 864,000 .
Ethiopia ndio nchi itakayopea kisi kikubwa katika kanaa hii ya dozi 8,928,000.
Tanzania na Burundi ndio nchi katika kanda hii ambazo hazijaagiza chanjo hiyo na hazimo katika orodha ya mataifa yanayotambuliwa na COVAX.
COVAX imesema inataraji dozi milioni 1.2 za chanjo ya Pfizer-BioNTech kuwa tayari kaika robo ya kwanza ya 2021 baada ya kukamilishwa kwa makubaliano ya utoaji wa chanjo hiyo .
Chanjo hiyo itapigwa jeki na nyingine kutoka kwa AstraZeneca/Oxford ambayo itakuwa tayari kuwekwa chini ya mpango wa COVAX katika kipindi hicho .
