logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Genge la wanaume 4 lalawiti mzee aliyekuwa ametoka kukata maji Murang'a

Pale walimuangusha chini na kumfanyia unyama ule wenye aibu kubwa mmoja baada ya mwingine   na kumuacha akiwa hali mahututi.

image
na Radio Jambo

Habari15 December 2021 - 02:17

Muhtasari


•Akiwa anayumbayumba kuelekea nyumbani, wanaume wanne wenye umri wa ujana walimjia na kumkokota hadi eneo lililojificha.

•Pale walimuangusha chini na kumfanyia unyama ule wenye aibu kubwa mmoja baada ya mwingine   na kumuacha akiwa hali mahututi.

crime scene

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 41  amelazwa katika hospitali moja kaunti ya Murang'a akiwa hali mahututi baada ya kulawitiwa na genge la jamaa wanne 

Mhasiriwa alikuwa anatembea kuelekea nyumbani kwake katika kijiji cha Githiagara, kaunti ndogo ya Kigumo  mwendo wa saa saba usiku wa kuamkia Jumanne wakati masaibu yale yalimpata. Alikuwa ametoka kukata maji na wazee wengine.

Akiwa anayumbayumba kuelekea nyumbani, wanaume wanne wenye umri wa ujana walimjia na kumkokota hadi eneo lililojificha.

Pale walimuangusha chini na kumfanyia unyama ule wenye aibu kubwa mmoja baada ya mwingine   na kumuacha akiwa hali mahututi.

Kufuatia hayo jamaa wawili, Bernard Kamande (25) na Erick Kimani (21) walikamatwa baada ya mhasiriwa kuwatambua. 

Wawili hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Muthithi huku msako wa wenzao wawili ukiendelea.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved