logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Nimekuwa muigizaji rasmi!" Magix Enga afichua ukweli kuhusu madai yake ya Illuminati

Baada ya kufanikiwa kuwadanganya Wakenya wengi, mzalishaji huyo amejipiga kifua kuwa mwigizaji mahiri na kuwasihi watu wamwache afanye mambo yake jinsi anavyotaka.

image
na Radio Jambo

Michezo31 January 2022 - 03:00

Muhtasari


•Enga ameweka bayana kuwa yote aliyosema akiwa kwenye  mahojiano na Presenter Ali yalikuwa mzaha tu wala sio ukweli kuhusu maisha na utajiri wake.

•Baada ya kufanikiwa kuwadanganya Wakenya wengi, mzalishaji huyo amejipiga kifua kuwa mwigizaji mahiri na kuwasihi watu wamwache afanye mambo yake jinsi anavyotaka. 

Mwanamuziki na mzalishaji tajika nchini Magix Enga amejitokeza kueleza kuwa madai ya kuwa mwanachama wa zamani wa Illuminati ambayo alitoa hapo awali yalikuwa ya kusaka kiki tu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Enga ameweka bayana kuwa yote aliyosema akiwa kwenye  mahojiano na Presenter Ali yalikuwa mzaha tu wala sio ukweli kuhusu maisha na utajiri wake.

Msanii huyo amedhihirisha alitumia umaarufu ambao alipata kufuatia madai aliyotoa kuachilia vibao vitano kwenye Youtube channel yake na vimeendelea kutazamwa sana.

"Hii video ya kuchekesha bado inavuma vipi??  Inapeleka mzaha katika hatua nyingine.  Hakuna njia fupi katika maisha haya ,  fanya bidii rafiki yangu na uombe. Lakini illuminati ni kweli kwa wale wanaoamini. Nilikuwa nikisikia kuwahusu pia kama nyinyi. Asanteni kwa kutazama. Nilitoa video 5 za muziki kwenye YouTube yangu" Enga alisema.

Baada ya kufanikiwa kuwadanganya Wakenya wengi, mzalishaji huyo amejipiga kifua kuwa mwigizaji mahiri na kuwasihi watu wamwache afanye mambo yake jinsi anavyotaka. 

"Bado niko na miaka ishirini na kitu na nina nyimbo nyingi kubwa kwenye YouTube na nabaki kuwa mtayarishaji bora/Msanii bora Afrika. Unatarajia nini kama sio vichekesho tupu na muziki mzuri. Wacheni mtoto afanye mambo yake bila chuki." Enga amesema.

Hivi majuzi Magix Enga alijitokeza kudai alijiunga na Illuminati akiwa na umri wa miaka 23 na hivyo ndivyo aliweza kujinufaisha kiusanii.

Alidai kwamba bado anawindwa na wanachama wa kikundi hicho baada ya kugura alipotakiwa kutoa vitu ambavyo hangeweza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved