logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Aliyekuwa mbunge William Kisang ashinda uchaguzi wa useneta wa UDA Elgeyo Marakwet

Katika kura za mchujo za UDA Jumamosi Kisang alipata kura 28,126 mbele ya wapinzani wake Tim

image
na Radio Jambo

Uchaguzi27 November 2022 - 08:00

Muhtasari


  • Kisang alisherehekea matokeo ingawa wapinzani wake walikataa matokeo hayo kwa madai kuwa kulikuwa na dosari kubwa

Aliyekuwa mbunge wa Marakwet Magharibi, William Kisang, aliwashinda wagombea wengine 20 wa kiti cha mchujo wa UDA katika mchujo wa useneta wa Kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Huku UDA kikiwa chama kikuu zaidi katika eneo hili, Kisang anachangamoto ya kuchaguliwa kuwa Seneta mnamo Januari 5 2023 kupitia uchaguzi.

Uchaguzi huo ulitokana na kujiuzulu kwa Waziri wa Barabara Kipchumba Murkomen ambaye alikuwa amechaguliwa Agosti 9 lakini akajiuzulu baada ya kuteuliwa na Rais William Ruto.

Katika kura za mchujo za UDA Jumamosi Kisang alipata kura 28,126 mbele ya wapinzani wake Tim Kipchumba na Jonah Tanui aliyepata kura 26,756 na 26,735 mtawalia.

Kisang alisherehekea matokeo ingawa wapinzani wake walikataa matokeo hayo kwa madai kuwa kulikuwa na dosari kubwa.

“Namshukuru Mungu kwa ushindi huo na nina furaha kwamba mapenzi ya wananchi yamekuwepo,” alisema Kisang.

Nicodemus Bore ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi alitangaza Kisang kuwa mshindi na kupewa cheti cha chama.

Kisang ambaye alihudumu kama mbunge kwa mihula miwili huko Marakwet Magharibi ameshindwa katika uchaguzi wa Agosti lakini akasema anashukuru Mungu amemfungulia mlango mwingine.

"Ninaahidi kuwatumikia watu wetu kwa kujitolea na maono makubwa kwa kaunti yetu", alisema.

 

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved