Wakaazi wa Sondu kaunti ya Kisumu wanaitaka serikali kuingilia kati kufuatia mapigano yaliyosababisha vifo vya watatu Jumanne usiku.
Mapigano hayo yalitokea Jumanne usiku katika mpaka wa Kericho-Kisumu karibu na soko la Sondu.
Wakazi hao wakizungumza na vyombo vya habari siku ya Jumatano walisema wanapata riziki zao kutoka soko la Sondu na kwamba mapigano hayo yamewavuruga shughuli zao za kuwaingizia kipato.
"Mimi naishi Sondou na sisi wanawake, Sondu ndo mahali petu pa ukubwa. Na sahii hatuezi ukubwa, tunakufa njaa," mwanamke mmoja alisema.
Waliuliza viongozi wao wanafanya nini kuhusu mapigano hayo ambayo yalikuwa yanawadhuru na kuwaacha wengine wakiwa wamekufa.
"Na hawa viongozi kwa nini wasitusaidie? Wanatuua kama kuku, MCA uko wapi? Ojienda uko wapi? Nyong'o uko wapi? Tunaumia. Sisi wanawake sisi ndo tutaumia sababu sisi ndo tunatafuta vile watoto wanakula," mmoja wa wakazi alisema.
Baadhi ya waliojeruhiwa wakati wa makabiliano hayo wamelazwa katika hospitali kwa ajili ya matibabu.
Polisi walisema magenge yanayodaiwa kuwa na pinde na mishale yalivuka kutoka kaunti jirani na kuwashambulia wakaazi katika soko la Sondu na karibu na soko.
Magenge hayo yanadaiwa kuiba majumba pia.
Sondu ni mji mdogo wa mpaka kati ya kaunti za Kisumu na Kericho.
Mpaka kati ya kaunti za Kisumu na Kericho umekuwa na utata kwa miaka mingi huku mpaka wa awali ukidaiwa kuwa nyuma ya kituo cha Polisi cha Sondu kilichokuwa katika Kaunti ya Kisumu.
Mnamo 1992, mpaka ulirudishwa hadi Kaunti ya Kericho