Kuku wakiwa wengi wana mwaya mtama kwenye kitengo cha toboa siri, katika toboa siri ya kwanza mwaka huu mwanamke mmoja aliwacha ashabiki wa radiojambo midomo wazi baada ya kutoboa siri yake.
Kulingana na mwanamke huyo alimuacha aliyekuwa mume wake, kwa ajili ya baba yake mdogo.
Je sababu kuu ya kumuacha ni ipi?
"Nilikuwa na mpenzi ambaye alikuwa mume wangu, alinitambulisha kwa baba yake mdogo, mimi niliona ni kama tu baba mkwe
Siku moa alinipigia simu na kuniambia kwamba kuna kitu anataka tuzungumze naye, nilipoenda kwenye hoteli niliata ameagiza mapochopocho
Tulienda kwenye chumba cha wageni, ndio alisoma katiba mzuri kuliko mume wangu, nataka nimtobolee siri nimwambie kwamba aache kunipigia simu na kuniuliza sababu ya kumuacha, nilimuacha kwa ajili ya baba yake mdogo ambaye anasoma katiba vyema kumshinda kwa hivyo awache kunisumbua," Alieleza mwanamke huyo.