logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanaisho: Jamaa amuacha mpenziwe kijijini, atorokea mjini kisha alia katelekezwa

Alinipa mtoto akaniacha Western yeye akaenda Nairobi, ajue ni ya wajanja

image
na TOM KIRIMI

Vipindi13 June 2023 - 06:42

Muhtasari


  • • Nilikosana na yeye mwezi wa nane last year baada ya yeye kusikia fitina za watu kwamba nimeoa ilhali mimi niko single sijaoa. Nilimpigia simu jana usiku saa sita pia baada ya Mama Mkwe kusema eti mimi namchezea so Bibi aka lose hope.
  • •Mimi nimeongea na yeye, angekuwa mtu serious anataka bibi, huwezi julisha bibi ako mahali fulani anataka waonane?
Ghost na Gidi

Katika kitengo cha patanisho, John Barasa, 26, ameomba kupatanishwa na mchumba wake Elizabeth Namusia, ambaye analenga kumuoa baada ya kuchumbiana kwa kipindi cha miaka miwili.

John, ameeleza kuwa walikosana na Elizabeth mwaka jana, kutokana na visingizio na fununu kutoka kwa watu kwamba alikuwa na uhusiano kutoka kwa bibi mwingine na tayari alikuwa ameoa. Mama mkwewe pia alichochea kuwa alikuwa akimcheza Elizabeth, jambo ambalo lilimghadhabisha sana likichochea kukosana kwao. 

“ Mimi ni John Baraza 26yrs kutoka Bungoma. Ningependa mnipatanishwe na Bibi yangu ambaye tumepanga kuoana anaitwa Elizabeth Namusia 24yrs. Tumekuwa kwa uhusiano kwa miaka miwili na ako na mtoto moja ambaye alikuja naye. Nilikosana na yeye mwezi wa nane last year baada ya yeye kusikia fitina za watu kwamba nimeoa ilhali mimi niko single sijaoa. Nilimpigia simu jana usiku saa sita pia baada ya Mama Mkwe kusema eti mimi namchezea so Bibi aka lose hope. tafadhali naomba mniongolee kabla hajamove.”

Katika mawasiliano na Radio Jambo, Elizabeth alikiri kwamba bado angali anampenda John kama mchumba wake, ila akijawa na maswali mengi sababu za mchumba wake kutorokea mjini.

“ Elizabeth, Mbona umenipeleka kwa radio jambo? wewe umenipelekaje kwa Radio Jambo? hivyo ndivyo umeamua? Mimi nimeongea na yeye, angekuwa mtu serious anataka bibi, huwezi julisha bibi ako mahali fulani anataka waonane?” Aliuliza Elizabeth.

Aliendelea kueleza kwamba hana shida naye ila anachohiitaji kutoka kwake ni awache ujanja amchukue kama mpenzi wake. “Mimi sina shida na John, ni mume yangu nampenda lakini vitu mimi siataki aache ujanja ajue mii ni mke wake na bado namhitaji.”

John aliendelea kusema kuwa mapenzi yake yalimfanya ampeleke redioni ndiposa Wakenya wengi washuhudie na wasikie kwamba bado angali anampenda.“ Nilikuchagua wewe kama bibi yangu, ninhali nakupenda sana kama mke yangu, upendo wako umefanya nikulete Radio Jambo Wakenya wote wajue nakupenda.”

Ungewashauri vipi wapenzi hawa wawili?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved