logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: "Nilifikiria hajui password yangu, nashangaa!" Jamaa ashtuka baada ya mkewe kuchunguza simu yake, kumshika aki'cheat

"Mteja aliniambia nisimamishe gari, mimi nilifikiria mteja anataka kuenda haja ndogo, nikasimamisha gari. Tulikuwa tunapiga mastori tu,' Denis alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho23 October 2024 - 08:43

Muhtasari


  • Denis alidai kwamba mkewe alimpata akiongea na mwanadada mwingine ndani ya gari yake na akawa anashuku anatoka nje ya ndoa.
  • Sharon alipopigiwa simu, aliweka wazi kwamba alipata jumbe za kutiliwa shaka kwenye simu ya mumewe.

Denis Onchuru ,27, kutoka Isinya alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Sharon Mokeira ,25, ambaye alikosana naye mwezi mmoja uliopita.

Denis alidai kwamba mkewe alimpata akiongea na mwanadada mwingine ndani ya gari yake na akawa anashuku anatoka nje ya ndoa.

"Mimi ni dereva wa teksi. Mke wangu alikuja akanipata na mrembo kwa gari. Nilimuelezea haniamini. Anasema niko na warembo wengi," Denis alisema.

Aliongeza, "Huyo nilikuwa naye alikuwa mteja. Nilimueleza hakuamini. Alinipata nikiongea na yeye kando ya barabara. Mteja aliniambia nisimamishe gari, mimi nilifikiria mteja anataka kuenda haja ndogo, nikasimamisha gari. Tulikuwa tunapiga mastori tu."

Denis hatimaye alikiri kwamba alikuwa na mahusiano ya nje.

"Enyewe ilikuwa naye lakini ilikuwa ni mahusiano kidogo tu," alisema.

Sharon alipopigiwa simu, aliweka wazi kwamba alipata jumbe za kutiliwa shaka kwenye simu ya mumewe.

"Nilipata meseji kwa simu yake, alikuwa anaongea na msichana mwingine. Ikawa inaleta shida. Ni mmoja tu nilipata," Sharon alisema.

Denis alimuomba msamaha akisema, "Nakuomba msamaha hajua nilikukosea. Turudiane tukae kama zamani. Kuja tuendelee kuzaa watoto wengi."

Sharon hata hivyo aliweka wazi kwamba hana muda wa kuzungumza na mumewe kwani alikuwa akienda mahali.

"Unaniharibia wakati," alisema kabla ya kukata simu.

Denis alisema, "Shida yake anakuwanga wa kukasirika ovyo ovyo. Alikuwa hajui password yangu, sasa nashangaa. Nilifikiria hajui password yangu, sasa nashangaa."

Gidi alimalizia kwa kumshauri Denis kuhusu jinsi ya kukaa kwenye ndoa, na kuendeleza kazi yake.

"Usikule stock na mteja tafadhali," alimwambia.

Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved