logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilipoteza hisia ya kunusa, Asema mjane wa Bob Collymore

Nilipoteza hisia ya kunusa, Asema mjane wa Bob Collymore

image
na

Patanisho02 October 2020 - 05:55
NA NICKSON TOSI

Kumpoteza mtu wa karibu maishani ni swala ambalo huwa na machungu haswa inapobainika kuwa huwa ameacha nafasi ambayo kuijaza huwa ni vigumu.

Mjane wa Bop Collymore, Wambui Kamiru ameelezea namna alivyoathirika kisaikolojia haswa kwa kupoteza hisia za kunusa (sense of smell) baada ya kumpoteza mumewe kupitia maradhi ya saratani.

Collymore aliaga dunia mnamo Julai mosi mwaka 2019.

Akiandika katika mtandao wa Twitter kuwa aliathirika pakubwa baada ya kumpoteza mumewe hali iliyomfanya kupoteza hisia zake za kunusa.

Kwa sasa, mjane huyo amesema kuwa imembidi kuvumulia machungu hayo na kukubali kuwa kifo ni safari ya kila mmoja.

"Hisia zangu za kunusa hazijakuwepo kwa muda sasa. Imefika mahali imenibidi kukubali kuwa kifo ni njia ya kila mmoja na sasa nimezoea," aliandika Wambui.

MHARIRI: Davis Ojiambo

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved