logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Rayvanny kwangu hatoki! Paula amjibu Fahyma

Paula na Fahyma wanazidi kumpigania Rayvanny, kila mmoja akitaka awe wake.

image
na Radio Jambo

Habari07 March 2022 - 07:17

Muhtasari


• Paula amshukiwa vikali Fahyma na kumuambia kwamba hawezi mpaka Rayvanny vile anavodai, amemuambia Rayvanny kwake habanduki hata kwa dawa.

Kwa kile kinachoonekana kama ni majibizano na ugomvi wa mtu na mke mwenza, Paula Kajala ameamua kurusha mkwara mzito ambao wengi wanasema unamlenga Fahyma ambaye juzi kati alimchamba kwelikweli.

Kwa muda mrefu sasa, wawili hao wamekuwa wakirushiana vijembe mitandaoni kuhusu tonge kwenye sahani, kwa maana ya Rayvanny ambaye anaonekana kung’ang’aniwa na wanawake hawa huku kila mmoja akijitahidi kuvuta upande wa kwake.

Ugomvi wao ulianza wakati Fayma ambaye ana mtoto mmoja na Rayvanny kutengana na msanii huyo na Paula kuchukua hatamu ambapo amekuwa akimpasha Fahyma kwamba hakuwa anajua kumdekeza Rayvanny lakini pia Fahyma si mchache wa kihivyo kwani anajua kujibu mipigo sawasawa.

Juzi kati wawili hao wamefarakana mitandaoni wakati Fahyma alisema kwamba akitaka Rayvanny amrudie atafanya hilo kwa dakika chache tu tena bila kusita kwani yeye ndiye anashikilia usukani wa halimashauri ya kichwa cha mwanamuziki huyo na kujigamba kwamba pia ana mtoto na yeye.

Paula sasa kwa kile kinachoonekana kama ni kujibu maneno hayo pia alijawa na ghadhabu na kujitupa kwenye insta stories zake ambqapo alitema nyongo kwa kusema kwamba Rayvanny kwake alishafika na kunata, jambo la kung’oka ni kama ndoto za alinacha.

“Kwangu habanduki, kwako hatoboki. Jamani wambeya habari zenu muwe na siku njema,” Paula alifuma kombora hilo kwa Fahyma.

Mpaka kufikia sasa msanii Rayvanny hajazungumza lolote kuhusu mfarakano wa wapenzi wake mitandaoni huku wngi wakihoji kwamba yupo katikati kwa sababu mwishoni mwa mwezi jana alimkanya mtangazaji Juma Lokole kwa kumtaka aache kuwazungumzia wapenzi wake na haswa Fahyma kwa sababu ni mama wa mtoto wake.

Kwa sasa Paula ambaye ni mtoto wa muigizaji mkongwe Frida Kajala yupo nchini Uturuki akisomea kitivo cha uuguzi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved