
Kupitia Instagram, Chino amefanya kufuru kwa kubadilisha picha ya wasifu wake na kuiweka ile ya Marioo, siku moja tu baada ya Marioo kumuandikia waraka mrefu akimlalamikia kwa kumdharaulisha kwenye jamii za mitandaoni.
Chino aliweka picha ya pamoja wakiwa wamekumbatiana na Marioo na kusema kwamba hakuna bifu kati yao.
Akiulizwa kuhusu bifu na shabiki mmoja, Chino aliweka wazi kwamba hamna bifu wala mfarakano baina yake na Marioo na kumtaja kama kaka yake mkubwa.
“Hakuna bifu kati ya kaka na mdogo bwake, mkubwa wangu,” Chino Wanamani alijibu.
Hii ni licha ya Marioo kuzua uvumi wenye ukakasi kwamba Chino alihusika katika jaribio la kumuua kwa kutumia sumu.
“Hii chuki imekuwa kubwa sana kiasi kwamba naanza kuamini kwamba pengine ni yeye alihusika kutuma watu waniwekee sumu ambayo nashukuru Mungu tulifanikiwa kuiwahi hapo siku zilizopita. Kwa sababu pia yapo maneno tunayoyasikia akisema kwamba kitu kinachomsumbua ni mimi kutajwa kwenye historia ya maisha yake, kweli ndio tumefikia huku?” Marioo alisema akiambatanisha na picha akiwa amelazwa hospitalini.
Wawili hao wamekuwa katika uhusiano baridi kwa muda sasa baada ya Chino kujitoa katika kikosi cha wacheza densi ambao walikuwa wanafanya kazi chini ya Marioo.




© Radio Jambo 2024. All rights reserved