logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Babangu Alikufa Kama Bado Sijamsamehe!” – Kennedy Rapudo

“Alipokufa nilikuwa shuleni na hakukuwa na simu ya kunitaarifu hivyo hata mazishi yake sikuhudhuria lakini baadae nilitembelea kaburi lake,” aliongeza.

image
na MOSES SAGWE

Burudani05 February 2025 - 12:44

Muhtasari


  • “Nimekulia maisha ya utotoni katika kaunti ya Migori mikononi mwa nyanyangu. Wazazi wangu walikuwa wametalikiana, kila mmoja alikuwa kivyake muda wote.”
  • Rapudo alisema kwamba kilichomfanya kuishi na kinyongo dhidi ya babake ni baba huyo kutomtafuta licha ya kujua alikuwepo.
caption

MFANYIBIASHARA Kennedy Rapudo kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu maisha yake ya awali kabla ya umaarufu wa mitandaoni, shukrani kwa mkewe Amber Ray.

Akizungumza na Dr Ofweneke katika podikasti ya Lessons @30, Rapudo alifichua kwamba hakuweza kufurahia maisha ya utotoni na wazazi wake wote, kwani walitengana akiwa na umri wa miaka 6.

Baba huyo wa watoto 3 alieleza kwamba babake aliondoka katika maisha yake na alikuja kukutana naye baadae akiwa katika shule ya upili, jambo ambalo lilimfanya kuishi na kinyongo naye.

“Nimekulia maisha ya utotoni katika kaunti ya Migori mikononi mwa nyanyangu. Wazazi wangu walikuwa wametalikiana, kila mmoja alikuwa kivyake muda wote.”

Rapudo alisema kwamba kilichomfanya kuishi na kinyongo dhidi ya babake ni baba huyo kutomtafuta licha ya kujua alikuwepo.

Alisema yeye kama tu mtoto mwingine yeyote wa kiume, katika makuzi huwa unaangalia na kufuata nyendo za baba lakini kwake hakukuwa na kitu kama hicho.

“Kukua bila baba kuliniathiri, unajua kama kijana mdogo unakua ukimtazamia baba, ukiwa shuleni unaona marafiki zako wanatembelewa na kina baba na wew babako hayuko, kwa kweli hilo linakuathiri kisaikolojia.”

“Iliniathiri sana kiasi kwamba hadi nilipofika darasa la 6-7 ilinibidi kuzungumza na mamangu kunionyesha babangu yuko wapi. Kwa sababu sikuwahi kumuona kutoka utotoni. Mama alisafiri hadi Mombasa kumtafuta lakini kwa bahati mbaya hakumpata na aliponiambia hapo ndipo nilikubali hali yangu kwamba baba hayupo maishani mwangu,’ Rapudo alisema.

Baadae katika shule ya upili baada ya kifo cha mamake, Rapudo alipata nafasi ya kuonana na babake lakini hilo lilimtia uchungu hata zaidi na kumchukia.

“Kusema ukweli mimi kuonana naye nilihisi kusalitiwa. Kwa sababu huyu jamaa alikuwa hai miaka hiyo yote na hakuwahi nitafuta na alikuwa anajua nipo. Na wakati hii nikimkuta tayari mamangu alikuwa ameshafariki. Hivyo hata kukutana kwangu na yeye hakukubadilisha chochote katika nafsi yangu,” Rapudo alimeza mate machungu.

“Alipokufa nilikuwa shuleni na hakukuwa na simu ya kunitaarifu hivyo hata mazishi yake sikuhudhuria lakini baadae nilitembelea kaburi lake,” aliongeza.

Kuhusu iwapo alikuja kubadili mtazamo na kusameheana na baba mzazi, Rapudo alisema;

“Alihisi amenikosea, alijaribu kuniomba msamaha ilikuwa vile ilikuwa wakati huo. Kwa bahati mbaya alifariki kabla nimsamehe na hivyo hatukuweza kutafuta mwafaka wa amani,” Rapudo alifunguka.

Alisema kwamba uhusiano baridi kati yake na babake ulimpa funzo kuu katika maisha na ndio maana anafanya jitihada zote kuwepo katika maisha ya wanawe licha ya kuwazaa na kina mama tofauti.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved