
ALIYEKUWA msanii wa Gengetone, Peter Miracle Baby amefichua kwa nini hawezi rudi tena katika uimbaji na utunzi wa mirindimo hiyo.
Akizungumza kwenye podcasti ya Nguthii, Miracle Baby alisema
kwamba Gengetone ilikuwa inaelekea kuua vijana na kusema kwamba yeye kama mmoja
wa hao vijana, hawezi rudi katika ‘mauti’ hayo.
Miracle Baby alisema kwamba kwa sasa yeye atasalia tu katika
kuimba muziki wa Mugithi na kueneza injili, akitabiri Gengetone iliyofufuka
kufariki tena kabla mwaka huu kuisha.
“Gengetone ilikuwa
inaenda kumaliza vijana, ilikuwa inauwa watu, hivyo mimi siwezi rudi kwa kitu
chenye kilikuwa kiniue,” Miracle Baby alisema.
“Gengetone ilikuja kisha
ikaisha, hivyo huwezi niambie nirudi kwa kitu chenye kilikuja na kisha
kikaisha. Sikudanganyi, Gengetone haimalizi huu mwaka, haiwezi rudia. Hivyo kama
hatutakuja na mkakati mwingine sioni kama kuna maana yoyote tunafanya katika
hii sanaa,” aliongeza.
“Hatuwezi ishi place moja,
baana joo tunazidi kuzeeka ..izo doba ziachiwe up coming wajijenge vile tu
zilitujenga tusipo do ivo tutaishi na millions of views bt kwa mfuko zero...for
now acha ni pige gospel mugithi zangu.”
Msanii huyo alisema kwamba Gengetone ilikuwa inatumia lugha
chafu na haiwezi kudumu kwa muda mrefu kwa sababu watu waliokuwa wanaipenda
kipindi kile sasa hivi wameshakomaa kiakili na hawataki tena kusikiliza kwa
lugha chafu ambayo ilikuwa inatumika kwenye miziki hiyo.
“Vijana wenye tulikuwa
tunaimbia Gengetone kitambo sasa hivi ni watu wako na familia wanatafuta kazi. Hao
sasa si wenye tutakuwa tunaimbia, hao watataka tuwaambie vitu vya kupata kazi,
venye watapata pesa. Lakini ukisema niimbe tena kuhusu makalio ina maana
ninarudi kuimbia tena wenye wako kidato cha 4 sasa, hapo sasa nitakuwa naenda
mbele ama narudi nyuma?” Miracle Baby alijieleza.
Miracle Baby alisema kwamba hadhira ya Gengetone ambayo
ilikuwa inapenda miziki ya kuzungumzia makalio na viuno vya wanawake sasa ni
watu wazima wanataka kusikiliza michongo ya kusaka hela na Imani ya kuishi
kuiona kesho.
“Sasa hivi nimeamua
kukwama kwa Mugithi na pia kama nitaimba hizo zingine haitakuwa Genge, nitakuja
na muziki wangu kivyangu, muziki yenye mtu anaeza sikiliza impe motisha kwa
maisha,” alisema.
Hii hapa video akizungumza;