
MSANII kutoka Guinea, Grand P amelalamika baada ya kupokea kauli za kejeli kwamba mpenzi wake mpya nim toto sana kwake kutoka kwa wale waliokuwa wakimcheka kwamba mwanasosholaiti Eudoxie Yao hakuwa size yake.
Akipeleka kwenye ukurasa wake wa Facebook,
Grand P alisema kwamba hajui watu wenye chuki huwa wanataka nini kwani wao ndio
walikuwa wanamcheka kuwa Eudoxie Yao ni mkubwa sana kwake na sasa baada ya
kupata wanayetoshana, bado watu wameibuka na kejeli kwamba ameoa mtoto.
“Ufike wakati mkome sasa watu wangu,
wakati nilipost Jirani yangu (Eudoxie Yao), mliongea sana hadi mkachoka mkisema
sio size yangu. Nilikubali ukosoaji wenu. Sasa nimepata ambaye ni size yangu na
mumeleta kauli eti nimeoa mtoto. Watu wenye chuki sana nyinyi... kueni na siku
njema,” Grand P alisema.
Katika picha hiyo, alikuwa ameshikana na
mpenzi wake mpya ambaye alimtambulisha siku ya wapendanao kwa jina Mariame
Kaba.
Kijana huyo amekuwa
katika miaka ya nyuma kwenye uhusiano na sosholaiti wa Ivory Coast Eudoxie Yao
ambaye ana umbile kubwa maradufu kumliko Grand P.
Uhusiano wake na Yao
ulionekana kutumbukia mchangani mapema 2023 ambapio kufikia Aprili, alitangaza
kuingia katika penzi la mwanadada mwingine aliyeitwa kwa jina Yubai Zhang.
Grand P alitangaza
mahusiano yao kupitia akaunti yake ya Facebook akithibitisha mapenzi yake na
mrembo huyo wa Kiasia na kuweka wazi kuwa hakuna nafasi ya watu wenye wivu
maishani mwao.
"Yubai Zhang
wangu, hakuna nafasi kwa watu wenye wivu," alisema chini ya picha zake na Zhang alizochapisha Facebook.
Balozi huyo wa Guinea
nchini Mali alikatisha mahusiano yake na mwanamitindo Yao mwaka wa 2021 baada
ya kuwa kwenye mahusiano na mwanamitindo huyo kwa takriban miaka mitatu.
Wawili hao walitangaza
kukuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka wa 2020 baada ya kuchapisha picha
wakiwa pamoja.