
RAIS William Ruto ameonekana kuvutiwa na jinsi Wakenya wamekuwa wakibuni majina ya kumrejelea na kusema kwamba haoni ubaya katika majina hayo
Akizungumza katika siku yake ya 3 kwenye
ziara ya wiki moja kwenye kaunti ya Nairobi huko maeneo bunge ya Kibera na Lang’ata
Alhamisi, Ruto alisema kwamba Wakenya hawajaanza sasa kumbandika majina hayo.
Kiongozi huyo ambaye alionekana kuwa
mwingi wa furaha aliwaambia Wakenya kwamba watamuua kwa majina, akichukua fursa
hiyo kuimba kionjo cha wimbo wa ‘Kasongo’ – moja ya jina ambalo amebandikwa.
“Wacha niwaulize nyinyi Nairobi,
Langata... si nyinyi mtaniua na majina?”
Rais aliuliza kwa utani.
Kiongozi huyo wa nchi alitaja baadhi ya
majina ambayo amekuwa akibandikwa na Wakenya, si tu baada ya kuwa rais bali pia
huko nyuma hata kabla ya kuwa rais.
“Sasa mimi nataka niwaulize, mlianza
huko mkasema Hustler, halafu mkasema Survivor, kisha mkaenda jina lingine,
Zakayo. Sasa nimesikia mmeongeza lingine, Kasongo. Sasa haya majina mtaongeza
hadi yafike mangapi? Eeh? Bado mtaongeza lingine ama hayo yametosha? Haki nyinyi
mko na maneno. Sasa nyinyi mnataka haya majina yangu yafike mangapi?”
“Mnataka yafike 10? Sasa nitaongeza
William Kipchirchir Samoei Ruto Hustler Survivor Zakayo Kasongo...sijui nani. Anyway,
ni sawa tu. Tuendelee. Ama mnasemaje bwana?”
rais Ruto alitania.
Baadae katika eneo la Toi, rais Ruto
aliwapakulia wanafunzi msosi wa Chapati na kutaarifiwa kwamba tayari Wakenya
wamebuni jina lingine kumrejelea kama ‘El Chapo’ – jina ambalo alisema nis awa kwake
pia.
“Hata hiyo ya chapo pia nis awa,” rais
Ruto alisema huku akiwapakulia wanafunzi chapati.
Rais amekuwa akizuru maeneo na kuzindua
miradi mbalimbali katika kaunti pana ya Nairobi tangu Jumatatu wiki hii.