Wanamgambo wa Al-Shabaab. | picha: the-star.co.ke
Maafisa wa usalama wa Kenya wametibua jaribio la wapiganaji wa Al Shabaab kushambulia kijiji kimoja huko Ijara katika kaunti ya Garissa kinachojulikana kama Yumbis.
Wapiganaji hao walijaribu kupeperusha bendera yao katika vijiji vya Yumbis na Welmarer kabla ya wenyeji kuwaarifu maafisa wa usalama.
Wanamgambo hao waliteka nyara vijiji hivyo Alhamisi jioni baada ya kuwazidi nguvu maafisa wa polisi wa utawala katika eneo hilo.
Hakuna yeyote aliyejeruhiwa katika shambulizi hilo.