Aliyekuwa muigizaji wa machachri Tyler Kamau Mbaya almaarufu Baha kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram aliweza kumkumbuka mama yake ambaye alikuwa muigizaji wa humu nchini kwa ujumbe kuwa anampeza sana.
https://www.instagram.com/p/CF6uEJhDXUP/
Mama yake Baha alifahamika kama Beth Nyamura almaarufu Wanade katika kipindi cha mother-in-law ambacho hupeperushwa katika runinga ya Citizen.
Wanade alipoteza maisha yake mnamo mwaka wa 2013 baada ya kuugua saratani.
Baada ya kuposti picha ya mama yake aliandika ujumbe huu.
"Akina mama ni zawadi bora kutoka kwa Mungu, nakupeza sana." Aliandika Baha.https://www.instagram.com/p/CF6x0AmDu9q/
Aliaga dunia muigizaji huyo akiwa katika kidato cha kwanza katika shule ya upili ya Nairobi, baada ya miaka miwili Baha na ndugu yake walimpoteza baba yao na kuwa yatima, tangu siku hiyo wawili hao wamekuwa wakitia bidii katika kazi zao na kushikana mkono kwa kila jambo.