Mtangazaji maarufu wa Radio Jambo na mfuasi mkubwa wa mtindo wa kirasta Mbusi amesimulia safari yake katika fani ya usanii hadi kujipata katika redio .
Mbusi ambaye alikuwa akihojiwa na MC Jessy katika kipindi chake cha Youtube cha Jessy Junction amezua ucheshi sana kuhusu safari ya kujipinda ya maisha yake kuanzia alivyokuwa akifanya kazi ya kuigiza katika National Theatre hadi alvyopata kazi katrika kituo cha Gheto Radio . Amesimulia kwamba haikuwa rahisi kuingia redioni moja kwa moja kwani kuna wakati alilazimika kuuza ‘Mmea’ ambao anauita ‘Ngwelo’ ili kujikimu pamoja na familia yake kwani wakati huo mkewe alikuwa mja mzito
Kinyume na wengi wanavyofikiri kwamba safari yake ya redioni ilikuwa rahisi Mbusi amesema kwamba kwa miaka miwili unusu alikuwa akifanya kazi ya utarishi ama Messenger pale Gheto radio ambapo mshahara wake ulikuwa shilingi 3000 .
‘ Ningengoja kulipwa mwisho wa mwezi .lakini walikuwa wanasahau kama ninafaa kulipwa ….so ikifika tarehe 15 huko ndio nauliza malipo kisha mtu anaingia kwa mfuko yake ananipea mshahahara wangu’ alisema Mbusi huku akimuacha na kicheko kizito Jessy ambaye hakuamini kwamba Mhusi aliyapitia yote hayo .
Baada ya fursa kupatikaa Ghetto Radio Mbusi amesema aliendelea kufanya kipindi na wenzake hadi fursa ya kuingia Radio Jambo ilipofika . Anasema hakuna yeyote aliyetaka kuhama naye kuja Radio Jambo na alipata tatizo sana wakati huo kumtambua mmoja wa wenzake ambaye angekuja naye katika kituo hicho cha Radio Africa .Baadaye ,amesema mwenzake Lion , ndiye aliyepiga moyo konde na kuamua kuhama naye kuja Radio Jambo na kuanzisha kipindi cha Mbusi na Lione Teke Teke . Mbusi pia amekana ripoti ambazo zimekuwa zikisambazwa mitandaoni kwamba donge alilopewa kujiunga na Radio Jambo ni zito sana . Amesema pesa anazolipwa ni nyingi lakini sio kiasi ambacho hutajwa katika ripoti hizo .





 © Radio Jambo 2024. All rights reserved
© Radio Jambo 2024. All rights reserved