Msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz amewajibu wanaotaka aondolewe kwenye tuzo za BET akisema ni mawazo yao na anayaheshimu.
Staa huyo alisema kwamba mtu amseme wala amtukane hayo yote anashukuru.
Akizungumza na runinga ya Wasafi msanii huyo alikwa na haya ya kusema;
“Mimi naheshimu mawazo ya kila mtu, mtu akinifurahia, akinitukana akinisema mimi nashukuru
“Epuka sana kumchukia mtu anayezungumza kitu kibaya juu yako, huwezi kujua kaamka kavurugwa hasira zake na kaamua kukumalizia wewe, kesho mwenyewe akikaa atajuta na kukuomba msamaha,” Diamond Alizungumza.
Pamoja na wasanii kumuunga mkono Diamond katika kile kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kumpigia kura katika tuzo za BET alizochaguliwa kushiriki, baadhi ya wadau wanaona hastahili kuungwa mkono.
Wadau hao wamemkemea waziwazi kupitia mitandao ya kijamii wakidai kuwa hajalitumia vema jina lake la msanii mkubwa kukemea maovu, badala yake amekuwa akifanya mambo yake binafsi.
Mapema mwaka huu Diamond alivuma sana mitandaoni baada ya kutoa kibao chake cha 'Waah' akimshirikisha msanii wa Rhumba Koffi Olomide.
Ni kibao ambacho kilivunja rekodi kwenye youtube baada ya kuokea watazamaji wengi kwa muda mfupi.
Hii hapa video ya mahojiano hayo;