
Mchekeshaji maarufu wa Kikamaba Nicholas Kioko alisimulia historia ya Maisha yake tangu alipokuwa mdogo.
Nicholas Kioko alikuwa akihojiwa na kituo kimoja cha radio nchini wakati ambapo alisimulia usuli na asili ya maisha yake. Kioko alizaliwa gatuzi la Machokos eneo bunge la Yatta, alijiunga na shule moja ya msingi na kusoma hadi shule ya upili katika kidato cha pili kabla ya kufukuzwa shuleni na mwalimu mkuu kwa tuhuma za utomvu wa nidhamu.
Baada ya hapo Nicholas alikuja jiji kuu la Nairobi na kujiunga na light academy wakati ambapo alihitimisha masomo yake ya kidato cha nne.
Baada ya kutamatisha masomo yake Kioko aliazimia kuanza biashara ya kuuza maji, peremende na biskuti katika barabara kuu za kule Nairobi.
Kulingana na maelezo ya Kioko alipata wakati mgumu alipokuwa akiendesha biashara hiyo ni baada ya vijana fulani kuweza kumfukuza kutoka katikati ya jiji na kumwacha akiwa katika hali ngumu ya maisha.
Aliamua kwenda katika kituo kikuu cha mabasi cha Machakos mjini Country Bus wakati ambapo aliendeleza biashara hiyo ambapo alielezea kuwa alikuwa akipata riziki ya kila siku bila matata yoyote na kwa kuhakikisha kuwa yuko imara kimaaisha.
Baadaye alipewa wazo na rafiki yake mmoja aliyemwambia kuwa angependa kumwonyesha jinsi ya kutoboa akina dada masikio ili kuongeza urembo na aweze kuwa anaitekeleza kazi hiyo wakati ambapo anahisi yuko sawa.
'' Baada ya kutoka mjini kwa barabara niliazimia kuja kwenye kituo cha mabasi ya kuenda Magharibi na Nyanza ili kurahihisha kazi yangu nikiwa huko.
Ninafurahia kwa sababu nilipata rafiki yangu mmoja aliyeazimia kunipa maarifa na ujuzi zaidi nikajifunza jinsi ya kuwatoboa wasichana masikio na kuwapaka hina kwa kucha zao.
Hiyo kazi ilinisaidia pakubwa sana na iliniwezesha kupata takribani shilingi 80,000 ambapo niliweza kufanikisha ndoto yangu ya kusomea uanahabari katika chuo cha NBS.
Baada ya masomo ya NBS alienda masomo ya nyanjani katika kituo cha Royal media ambapo alibahatika na kuwa msanii wa haiba wa kuchekesha watu baada ya kuandaliwa mkeka wa kukalia na Lulu Hassan.