logo

NOW ON AIR

Listen in Live

PATANISHO: Juzi chali fulani alinikatia nikamgonga na chupa!

PATANISHO: Juzi chali fulani alinikatia nikamgonga na chupa!

image
na

Habari02 October 2020 - 03:06
Bi Mercy, 29, kutoka Eldoret anaomba apatanishwe na Kevo 39, ambaye walikosana mwaka mmoja uliopita.

"Tulikuwa tunaishi na yeye halafu tulikuwa tunakunywa pombe pamoja na kuna vile tukirudi kwa nyumba nilikuwa na kisirani, naleta fujo na kelele na ni jamaa mpole." Alisema Mercy.

Aliongeza,

Nilikuwa na ball ya miezi sita na mume wangu akanipiga na hasira na kwenda hosi ball ikatoka, sasa nimechoka na nikarudi nyumbani kwetu.

Wawili hao hawakuwa wameoana licha ya kuwa kwa uhusiano wa miezi mitatu, lakini walikuwa wanapangia kwenda kwa wazazi hadi alipogungua kuwa mpenziwe ni kisirani.

Mercy anadai kuwa wawili hao walizungumza wiki iliyopita ila bado hawajaelewana.

Ilifika wakati nikamwaga mafuta ya taa kwa nyumba akiwa amejifungia kwa bedroom hata kiberiti ndio ilikuwa imebaki. Imagine alikuwa hata ananipikia na mimi ndiye niliyemkosea.

Kevo hakujibu simu zetu na Mercy alipewa fursa amtumie mpenziwe ujumbe.

Ningependa kumwambia nampenda sana na najua nilimkosea na nikamsumbua. Lakini sijawahi hanya. Ilifika mahali akaniwacha kwa nyumba kwa miezi miwili.

Alikuwa analipa na ananilisha lakini hakuwa anakuja kwa nyumba. Siku moja nilimwita kwa nyumba lakini alikuwa na wasiwasi kwani alikuwa anaketi akisimama.

Kuna wakati nilikuwa karibu kumwagilia maji moto na alikuwa ananiogopa." Alisimulia Mercy akisema kuwa kwa sasa amewacha pombe.

Mercy anasema anamfikiria Kevo sana na hataki mwingine, isitoshe, juzi kuna jamaa alijaribu kumkatia naye kwa hasira alimgonga kwa chupa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved