Obado alidai kuwa haogopi chochote kwani atarudi kufanya kazi ya jua kali ambayo alikuwa anafanya kabla ya kuwa gavana wa kaunti hiyo.
"Sina lolote la kuogopa naomba afya jema ili niweze kuendelea na kazi yangu ya jua kali niliokuwa nafanya kabla niwe gavana nilikuwa nafanya mambo mengi ambayo hamna mtu yeyote anaulizia." Alisema Obado.
Gavana huyo alishangazwa na vile amekuwa kwenye vichwa vya habari hasa katika chama chake na hamna mtu yeyote anauliza alichokuwa anafanya kabala ya kujiunga na siasa.
"Wananionyesha kama mtu ambaye anaweza ishi kwa ajili ya ugavana, lakinii hawaulizi nilichokuwa nafanya kabla ya kuwa gavana."
Alisema haya mnamo Jumanne huku akiwatubiwa wanahabari,Baada ya kuachiliwa kwake baadhi ya wanachama cha ODM waliwakilisha mchakato wa kumuoondoa gavana huyo ofisini.