logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jubilee hakitamsimamisha mgombeaji katika uchaguzi mdogo wa Msambweni ODM-Tuju

Jubilee hakitamsimamisha mgombeaji katika uchaguzi mdogo wa Msambweni ODM-Tuju

image
na

Habari01 October 2020 - 09:20
TUJU
Chama cha Jubilee hakitamsimamisha mgombeaji katika uchaguzi mdogo wa Msambweniu  .

Kiti hicho kiliachwa wazi baada ya kifo cha   Suleiman Dori wa ODM.

Jubilee imesema kwa sababu ya ushirikiano wake na ODM hakitaweza kuwa na mgombeaji katika uchaguzi huo .

Chama hicho kimesema taifa kwa sasa linapitia  mambo mengi ikiwemo ushauri wa jaji mkuu David Maraga   kwa rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge .

" Kwa sasa nchi inapitia mengi na tunahitaji ukomavu  ili kuyashughulikia  ikiwemo kuziba mianya   katika mirengo ya kisiasa’. Amesema  katibu mkuu wa chjama hicho Raphael Tuju

Ameongeza ‘ Uamuzi huu umetolewa kwa wakati ufaao ili iwapo kuna mgombeaji wa Jubilee aliyetaka kiti hiki basi awe na njia mbadala za kugombea’

Wakaazi  wa eneo bunge hilo watamchagua mbunge mpya disemba tarehe 15  baada ya uchaguzi huo kuahirishwa kwa sababu ya janga la corona .

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved