logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Eric Omondi akejeliwa baada ya kumpendekeza Jimi Wanjigi kuwa rais wa Kenya

Kupitia kampeni iliyobandikwa jina 'Fagia wote', Eric amesema kuwa wakati umewadia

image
na Radio Jambo

Habari01 September 2021 - 12:49

Muhtasari


  • Eric Omondi akejeliwa baada ya kumpendekeza Jimi Wanjigi kuwa rais wa Kenya

Baada ya Mchekeshaji Eric Omondi kumpendekeza bilionea Jimi Wanjigi kuwa rais wa Kenya mwaka baada ya kustaafu kwa Uhuru Kenyatta mwaka ujao,wanamitandao wamemkejeli na kutoa hisia tofauti.

Kupitia kampeni iliyobandikwa jina 'Fagia wote', Eric amesema kuwa wakati umewadia kwa wale wote ambao wamekuwa uongozini kwa miaka mingi kuenda nyumbani na kuachia viongozi wapya usukani.

"Hatutaki majina zinajulikana. 2022 tunawafagia wote. Vijana tumeamka na tunakuja" Omondi alisema kwenye video aliyopakia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Omondi amesema kuwa kinara wa ODM Raila Odinga, naibu rais William Ruto, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzao wa ANC Musalia Mudavadi wameshindwa kusukuma nchi mbele na kuwataka wasiwanie viti hivyo mwaka ujao.

Hizi hapa baadh ya hisia za mwanamitandao;

karenzo.nyamu: Eric piga hustle. I hope amekulambisha fiti ama tumuanike πŸ˜‚πŸ˜‚

ngash4real: Hapo kwa Jimmy Wanjigi ndio umeanguka na tumbo

xclusivedeejay: So vijana we should rely on a 60 year old billionaire to help us ?? 🀦🏿‍β™‚οΈπŸ€¦πŸΏ‍β™‚οΈπŸ€¦πŸΏ‍♂️ vijana kweli tunapangwa tu kama kawa

charles_ndolo: πŸ˜‚πŸ˜‚ nilikuwa nafikiria kuna kitu ya maana mpaka nikafika hiyo part ya endorsement

kevinsky9: 😍so wanjigi or whatever his name is ni youthπŸ˜‚πŸ˜‚..enyewe uko na jokes.

babashawnpoetry: Ama unaadvertise kampuni ya vifagioπŸ™Œ

mariahkibs: Okay seriously??I thought kijana ni wewe.

ndungu_tosh: Jimi wanjigi amekuangushia kakiru mzuri sanaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

masila_justus: Kufagia iko sawa ,lakini hapo kwa jimmy wajingo ndio nguvu imeishia

sammykham: Kijanaa amelipwa πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logoΒ© Radio Jambo 2024. All rights reserved