Muigizaji wa Filamu za Bongo, Wema Sepetu amejitokeza na kueleza zaidi kuhusu posti aliyochapisha jana kwenye ukurusa wake wa instagram akiomboleza kifo cha Kaka yake.
Posti hiyo ilitafsiriwa vibaya na baadhi ya wanamitandao nchini Tanzania huku tetesi zikiibuliwa kuwa alikuwa anazungumzia Pofesa Jay.
Wema ambaye ni mshindi wa Miss Tanzania 2006, kutokana tetesi hizo zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, Alitumia instastori yake kueleza kuwa kinachotafsiriwa kwenye posti ni uongo na kueleza kama ingekuwa ni Profesa Jay angetoa habari zaidi.
“Huyu ndio niliemaanisha jamani.. msinielewe vibaya, ingekuwa vingine ningeandika habari zaidi,”alisema Wema Sepetu.
Profesa Jay amekuwa Hospitalini kwa takribani wiki nne, ambapo anaendelea kupokea matibabu.
Serikali ya rais Samia Suluhu iliahidi kugharamia matatibu ya Mwanamuziki Profesa Jay.