logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+video) Litboy anusurika kichapo baada ya densi ya kushtukiza kwa Maasai

"Ilinibidi nielezee kwa saa nzima kuwa huo ulikuwa mchezo wa kuchekesha." - Litboy

image
na Radio Jambo

Habari07 September 2022 - 12:23

Muhtasari


• "Hawakuona kamera kwa sababu mtu wangu wa kamera alikimbia, hakuna Matata,” Lit Boy

Mcheza densi za kushtukiza Olny Lit Boy ambaye jina lake halisi ni Ed Mbaria amejipata pabaya baada ya kujaribu densi ya kushtukiza kwa Maasai mmoja na karibu kupewa kichapo cha mbwa msikitini na kundi la Wamaasai waliokuwa wakiendesha biashara yao eneo hilo.

Lit Boy alipakia video hiyo akionekana akimkaribia Maasai huyo kwa densi na kisha kumrukia juu mgongoni kama nyani anavyoparamia mgomba wa ndizi.

Maasai huyo kwa mori anachomoa rungu yake na kwa kushirikiana na wenzake wanamkimbiza Lit Boy ambaye anatoka mbio kukwepa rungu ya mori ya Maasai.

Baadae alipopakia kwenye Instagram yake, Lit Boy alisema kwamab anawaonea Fahari sana watu wa jamii ya Maasai kwa ujasiri wao na ari ya kufanay kazi zao pendwa.

Alisema kwamba Maasai hapo walipomshika, ilimchukua zaidi ya saa moja kuwaelezea madhumni ya tukio zima na kuwahakikishia kwamba hakuwa na nia mbaya bali alikuwa anafanya mitikasi yake tu ya kuwashtukizia watu wa densi.

“Wamasai Wanafafanue Utamaduni wetu. Nashangaa nguvu zao na kutoogopa. Ilinibidi nielezee kwa saa nzima kuwa huo ulikuwa mchezo wa kuchekesha. Hawakuona kamera kwa sababu mtu wangu wa kamera alikimbia, hakuna Matata,” Lit Boy aliandika kweney ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na video ya tukio zima.

Mcheza densi huyo amekuwa kwa muda mrefu akizomewa kwamba anaiga mcheza densi mwenza Moya David kwa kuwashtukizia watu kwa densi ila mara kwa mara amekuwa akipuuzilia mbali madai hayo kwa kile anasema kwamba Sanaa ni kubwa sana kama nyama ya tembo na kila mtu ana haki ya kula kutoka upande wowote pasi na kung’ang’ania na mtu.

Itakumbukwa pia Moya David aliwahi kuelezea kwamba changamoto kama hiyo iliwahi mkumba siku moja alipofanya mzaa na Maasai na wakamkimbiza karibu kumpa kichapo kabla ya kujieleza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved