logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwijaku amuomba msamaha Ommy Dimpoz kwa kuibua mzozo wake na baba mzazi

Mimi nilichofanya sikutaka kukuchonganisha na mzee ili watu kuona labda huna mapenzi na mzee - Mwijaku.

image
na Radio Jambo

Habari16 September 2022 - 05:08

Muhtasari


• Ommy Dimpoz bana tusameheane. Mimi nilichofanya sikutaka kukuchonganisha na mzee - Mwijaku.

Mwijaku amemuomba msamaha Ommy Dimpoz kwa sakata la babake

Baada ya Sakata la msanii Ommy Dimpoz na babake mzee Faraji Nyembo kuzuka mitandaoni vikali, chanzo chake kilitajwa kuwa mtangazaji wa Clouds Mwijaku aliyemtafuta mzee huyo huko Sumbawanga katika tamasha lao la Fiesta.

Katika klipu yake, Ommy Dimpoz alisema kwamba Mwijaku alifanya yale mahojiano na mzee wake licha ya kuwa anajua stori yote kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Dimpoz alizungumza kwa uchungu mkubwa akituhumu Mwijaku kwa kutumia mzee Nyembo kama maudhui ya kufanya Fiesta yao itambe na suala hilo liionekana kumuathiri hata katika mambo yake ya kutafuta riziki.

Sasa baada ya Ommy kufunguka kwamba licha ya Mwijaku kujua ukweli wote, alienda mbele na kumkandia, mtangazaji huyo amekiri kweli alikosa na amemuomba radhi Dimpoz kwa madhara yote ambayo huenda zile klipu na mahojiano alifanya na mzee Nyembo zimemletea.

“Mimi kweli ninaijua stori kama ambavyo Ommy alisema kwenye klipu yake, kuenda kwa yule mzee ni sababu yeye aliniita. Katika mazungumzo yale nikafanya kumuambia mzee kwamba siku ile ilikuwa ya kuzaliwa kwa mwanawe Ommy Dimpoz na kwa kweli hilo lilimkwaza sana Ommy Dimpoz kwa hiyo, nikatumie nafasi hii kumwambia Ommy Dimpoz bana tusameheane. Mimi nilichofanya sikutaka kukuchonganisha na mzee ili watu kuona labda huna mapenzi na mzee, Hapana,” Mwijaku alisema.

Mtangazaji huyo pia alifichua kwamba aliwahi kumwambia mzee Nyembo ukweli kwamba alifanya makosa kumyima mapenzi ya mzazi mwanawe Omary Nyembo, almaarufu Ommy Dimpoz.

Mwijaku hakuishia hapo bali alirudi kwenye Instagram yake na kuachia ujumbe mrefu wa kumtaka radhi msanii Ommy Dimpoz kwa kile alichomfanyia. Alifunguka kwamba hata ule ujumbe alimtumia Ommy moja kwa moja na alifurahi ulipokelewa na kusamehewa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved