logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msanii Mbosso apata ajali ya barabarani akiwa Marekani

Msanii huyo alianza ziara yake ya kimuziki Marekani mnamo Februari 10.

image
na Radio Jambo

Habari15 February 2023 - 04:18

Muhtasari


• Mbosso alikuwa anajiandaa kwa ajili ya shoo yake ya Februari 17 katika jimbo la Colorado wakati ajali hiyo ilimkumba.

Mbosso apata ajali marekani.

Msanii wa miziki ya kizazi kipya kutoka Tanzania Mbosso ametangaza kuwa amepata ajali mbaya ya barabarani saa chache zilizopita akiwa nchini Marekani.

Mbosso ambaye wiki hii alianza ziara yake ya muziki nchini Marekani alipakia msururu wa picha na video kwenye instastories zake akionesha gari aina ya Landcruiser Prado ambalo alikuwa analitumiwa likiwa limegongwa vibaya upande wa mbele na pia kukwaruzwa maeneo ya kando.

Kwenye video moja, alionekana akipatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na maafisa wa trafiki wa Marekani huku picha nyingine ikionesha gari la kuvuruta magari mabovu likiwa tayari kulivuta gari hilo lililopata ajalai akiwa ndani mwake kuliondoa barabarani.

Mbosso aliwatoa mashabiki wake wasiwasi kwa kuwahakikishia kuwa hakupata kuumia vibaya sana mbali na maumivu kiasi ya baadhi ya sehemu za mwili wake.

“Alhamdulillah sijaumia sana. Ni maumivu tu kwenye mbavu upande wa kulia, bega na uti wa mgongo. Ila niko salama kabisa Alhamdulillah,” Mbosso alidokeza.

Msanii huyo kutoka lebo ya WCB Wasafi ya Diamond Platnumz alianza ziara yake ya kimuziki Marekani mnamo Februari 10 huko jimbo la Arizona, Februari 11 akaenda kule Seattle na Februari 17 anatarajiwa kuenda jimbo la Colorado japo haijulikani kama shoo hiyo itafanyika kutokana na ajali hiyo iliyomkumba Khan.

Taarifa Zaidi kuhusu hali yake ya afya baada ya tukio hilo itatolewa badae na uongozi wake, ila kikubwa mwenyewe kashazungumza kwamba yuko katika hali shwari.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved