
SERIKALI kupitia Wizara ya Ushirika na MSMEs imejitokeza kujitetea dhidi ya ripoti ya mkaguzi mkuu wa fedha za serikali Nancy Gathungu kuhusu ubadhirifu wa mkopo wa Hustler Fund.
Akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kitaifa ya Idara ya
Biashara, Viwanda na Ushirika ikiongozwa na Mhe. Maryanne Keitany, katibu
katika wizara hiyo inayoongzwa na waziri Wycliffe Oparanya, Susan Mang’eni
alikanusha vikali ripoti hiyo.
Wakati wa mkutano huo, Mang’eni alibaki na msimamo wa
serikali kwamba Hustler Fund ilikuwa imetolewa kwa watoto wadogo au wanufaika
wasiostahiki, akihakikishia kamati kwamba hakuna pesa zilizopotea au kutengwa
vibaya.
Pia alisisitiza uadilifu wa hazina hiyo, akikariri kuwa
huduma ya mkopo inasalia kuwa salama na imedhibitiwa kikamilifu.
“Takwimu zilizotumika katika
ripoti ya ukaguzi zilikuwa na makosa makubwa ya uchimbaji kwa sababu ukaguzi
haukufanyika katika mazingira ya moja kwa moja. Tangu wakati huo tumesafisha
rekodi, na watu wote waliochukuliwa sampuli wamethibitisha vitambulisho na
nambari za simu,” PS Mang’eni alieleza.
Wasiwasi ulijitokeza katika ripoti ya ukaguzi wa mwaka wa
fedha wa 2023/24, ikipendekeza kuwa baadhi ya wanufaika walirekodiwa kuwa ni
watu ambao hawajazaliwa, ambapo tarehe za kuzaliwa zilitarajiwa kuanzia Julai
2024 hadi Desemba 2073.
Hata hivyo, PS Mang’eni alitupilia mbali madai hayo, akieleza
kuwa tofauti hizo zilitokana na makosa ya uchimbaji wa takwimu badala ya
upotevu halisi wa fedha.
“Pia niliihakikishia
kamati kuwa mfumo wa Hustler Fund hauruhusu watoto wadogo kupata mikopo, na
hivyo kuimarisha dhamira ya serikali ya uwazi na uwajibikaji katika kusimamia
mfuko huo,” Mang’eni alisasisha kupitia jukwaa la X.