logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Duale: Ruto Atashinda Uchaguzi wa 2027

Duale alieleza kuwa serikali ya Kenya Kwanza itashinda kwa msingi wa rekodi yake ya maendeleo.

image
na Tony Mballa

Habari10 July 2025 - 10:09

Muhtasari


  • Jumatano, Ruto alidai kuwa upinzani unapanga njama ya kupindua serikali yake, akielekeza lawama kwa wanasiasa fulani ambao hakuwataja moja kwa moja lakini aliwatuhumu kwa kuchochea ghasia.
  • Kwa upande wake, Gachagua alikanusha madai hayo, akisema kuwa lengo la upinzani ni kumshinda Ruto kupitia kura mwaka wa 2027, na si kwa njia zisizo halali.

Waziri wa Afya Aden Duale amesema kuwa Rais William Ruto atashinda kwa urahisi katika uchaguzi wa urais wa 2027.

Duale alisema kuwa muungano tawala una idadi ya kutosha ya kura kuhakikisha Ruto anapata muhula wa pili madarakani katika uchaguzi ujao, licha ya wimbi la kauli za “muhula mmoja.”

Akizungumza katika mahojiano na Citizen TV siku ya Jumatano, Duale alieleza kuwa serikali ya Kenya Kwanza itashinda kwa msingi wa rekodi yake ya maendeleo.

“William Ruto atarudi kwa ushindi mkubwa… inshallah, muhula wake wa pili umehakikishwa,” alisema Duale.

“Atachaguliwa, si kwa sababu nyingine yoyote, bali kwa sababu atatimiza ahadi zake.”

Kauli zake zinajiri wakati ambapo kuna mvutano wa kisiasa kati ya Rais Ruto na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Gachagua amekosana wazi na Rais, akimtuhumu kwa kuipuuza na kuitenga eneo la Mlima Kenya.

Gachagua Sasa Atishia Kumpeleka Ruto ICC Kufuatia Amri ya Kuwapiga Risasi Waandamanaji

Gachagua na washirika wake wa upinzani wameapa kumng’oa Ruto mamlakani ifikapo 2027, huku madai yakiibuka kuwa wanahusishwa na maandamano ya hivi karibuni nchini.

Jumatano, Ruto alidai kuwa upinzani unapanga njama ya kupindua serikali yake, akielekeza lawama kwa wanasiasa fulani ambao hakuwataja moja kwa moja lakini aliwatuhumu kwa kuchochea ghasia.

Kwa upande wake, Gachagua alikanusha madai hayo, akisema kuwa lengo la upinzani ni kumshinda Ruto kupitia kura mwaka wa 2027, na si kwa njia zisizo halali.

“Hakuna mtu anayetaka kupindua serikali yako… tunataka kukukabili kwenye debe Agosti 2027, kwa hivyo tulia tu,” alisema Gachagua wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Mbunge Adai Chama cha Gachagua Kilichochea Ghasia Meru Siku ya Saba Saba

Alisisitiza kuwa vuguvugu la “Wantam” analoliongoza si harakati za mapinduzi, bali ni mwamko wa kisiasa unaolenga mabadiliko ya uongozi kwa njia ya kikatiba.

Gachagua pia alimuonya Ruto dhidi ya kutumia madai hayo ya vitisho kama kisingizio cha kuwanyamazisha viongozi wa upinzani.

Kauli ya Duale huenda ikaongeza mvutano unaoendelea wa maneno kati ya upinzani na wafuasi wa Ruto, huku pande zote zikijipanga kwa uchaguzi mkuu ujao.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved